NA MWANDISHI WETU
WATU wasiojulikana wamechoma msitu
wa Kirando wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ambao umeunguza miundombinu ya umeme ya
Shirika la umeme Nchini TANESCO.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
jioni hii Juni 24, 2017 na Kaimu Meneja Uhusinao wa TANESCO makao Makuu, Bi.
Leila Muhaji, imesema, uharibifu huo mkubwa wa miundombinu umeathiri
upatikanaji wa umeme kwa wateja wa maeneo ya Kirando na Kipili wanaopata huduma
ya umeme ya njia ya msongo mkubwa wa umeme unaopita kwenye maeneo hayo.
“Mafundi wa TANESCO waliofika kwenye
eneo hilo, wameshuhudia uharibifu mkubwa ambapo miundombinu ya umeme imeungua
na kusababisha hasara kubwa.” Alisema Bi Leila katika taarifa yake kwa vyombo
vya habari.
Bi Leila amesema TANESCO inawaomba
wananchi wote waishio kwenye maeneo hayo kutoa taarifa kwenye ofisi za TANESCO
au kituo cha polisi kilicho karibu ili kuokoa miundombinu ya umeme kwa manufaa
ya taifa.
Amesema, tayari vyombo vya ulinzi na
usalama kwa kushirikiana na TANESCO wameanza msako ili kuwabaini wahusika ili
sheria ichukue mondo wake.
Afisa wa polisi akiwa eneo la tukio huku akishuhudia jinsi moto huo ulivyoathiri nguzo za umeme
Hey, that’s really a good post on pets for sale in Delhi, i really like your blog as the information is very useful if you are a pet lover. Well, there is one more site for the same service www.helpadya.com you should check it for more detail.
ReplyDelete