August 16, 2017

Naibu Waziri Nishati na Madini amefanya ukaguzi Mradi wa Makambako - Songea



Naibu Waziri Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akipokelewa na wenyewe Kampuni ya JV Shandong Taikai Power LTD ambaye ni Mkandarasi anayejenga kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Makambako Agosti 15, 2017


Na Henry Kilasila

Naibu Waziri Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akiwa katika ziara za uzinduzi Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Tatu, amefanya ukaguzi katika Mradi wa Umeme Msongo wa Kilovolti 220 kutoka Makambako hadi Songea ili kujionea utekelezaji wa Mradi huo.

Dkt. Kalemani alisema Mradi huo umegawanyika sehemu tatu ambazo ni ujenzi wa Vituo vya kupoza na kusambaza umeme, ujenzi wa njia ya umeme Msongo wa Kilovolti 220 na usambazaji wa umeme katika Vijijji 120.

"Kinachofanyika tuna upgrade ili kuongeza nguvu ya umeme kutoka Kilovolti 132 hadi 220". Alisema Dkt. Kalemani.

Aidha, Mheshimiwa Waziri alitoa maelekezo yakimtaka Mkandarasi Kampuni ya JV Shandong Taikai Power LTD anayefanya upanuzi wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Makambako asitoke nje ya Mkoa wa Njombe hadi atakapokamilisha ujenzi.

Maelekezo mengine ni kuanza kazi mara moja na wasilipwe chochote mpaka kazi hiyo itakapofika kiwango cha kuridhisha

Kwa upande wa TANESCO aliutaka Uongozi kuhakikisha kufikia mwishoni mwa Mwezi Agosti Wateja wote walioomba umeme wawe wameunganishiwa.

Ujenzi wa Mradi wa Makambako Songea Kilometa 250 ulianza kujengwa Mwezi Desemba 2014 na unatarajiwa kukamilika Mwezi Septemba 2018.

Lengo la Mradi huu ni kusambaza umeme Vijijini ili kuchangia maendeleo ya Wananchi  katika Vijiji na Miji iliyopo katika Mikoa ya Njombe na Ruvuma.

Aidha, unafadhiliwa na Serikali ya Sweden kupitia Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA), Serikali ya Tanzania na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)

Ujenzi wa Mfumo wa usafirishaji umeme Makambako - Songea Msongo wa Kilovolti 220 unafanywa na Mkandarasi Kampuni ya Kalpataru Power Transmission LTD,

Mkandarasi JV Shandong Taikai Power Eng. LTD akijenga Vituo viwili vipya vya kupoza na kusambaza umeme Kilovolti 220/33kV vya Madaba na Songea pamoja na upanuzi wa Kituo cha Makambako 220/132/33kV.

Mkandarasi Isolux Ingenieria S. A akijenga mfumo wa usambazaji umeme wa Msongo wa Kilovolti 33 wenye jumla ya Kilometa 900, uwekaji wa Transfoma 250.

Aidha, Mkandarasi huyo anajenga mfumo wa Volti 400 katika Vijiji 120 na kuunganisha Wateja 22,700.

Naibu Waziri Nishati na Madini Mhe. Dkt. Medard Kalemani anaandamana na Wataalamu kutoka TANESCO, REA na Wizara ya Nishati na Madini katika Ziara hii ya uzinduzi wa Miradi ya REA Awamu ya Tatu ambapo ataendelea katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi, Arusha na Kilimanjaro.








No comments:

Post a Comment