Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa mradi wa uunganishwaji umeme wa Gridi ya Taifa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika Mkoani Lindi leo Mei 21, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Mradi huo sasa umeondoa kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa umeme ulio bora na wa uhakika kwenye mikoa hiyo ya Kusini.
NA MWANDISHI WETU, MAHUMBIKA-LINDI
WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
amewahakikishia watanzania wote kuwa Serikali itafikisha umeme kila kona na
kila kijiji.
Waziri Mkuu aliyasema hayo mara baada ya
kuzindua mradi wa uunganishwaji wa umeme wa Gridi ya Taika kwa mikoa ya Lindi
na Mtwara kwenye hafla iliyofanyika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha
Mahumbika mkoani Lindi leo Mei 21, 2018.
Hata hivyo aliwataka kuwa wavumilivu kwani
mipango ya serikali ambahyo ni kuhakikisha umeme unafika sio tu maeneo ya
mijini bali pia kwenye vijiji vyote vya Tanzania.
“Kitendo kinachofanyika hapoa leo ni ushahjidi
wa ahadi hiyo ya serikali na ninachowaomba Watanzania ni kuwa na subira kwani
serikali inatekeleza ahadi ilizotoa kuhakikisha watanzania wanapata umem wa uhakika
na wa bei nafuu.”
Akizungumzia uzinduzi huo ambao sasa umetoa sukuhisho la
uhaba wa umeme kwenye mkoa huo wa Lindi Waziri Mkuu alitoa maagizo kwenye
halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha maeneo yote nyeti ya huduma za kijamii
yanafikishiwa umeme ikiwemo shule na hospitali
“Hatutarajii kuwa na eneo lenye shida ya
umeme, hapa ni umeme masaa 24, na tafsiri ya serikali kuwa hapa ni umeme wa
uhakika na wa kutosha ndio hii ambayo leo hii tumezindua.” Alisema.
Alisema sera ya serikali ni ya uchumi wa viwanda,na
kwamba, wale watu wanaotaka kuwekeza viwanda vya Korosho, Salfa na vifaa
mbalimbaki kwenye mkoa wa Lindi sasa ni wakati wao kwenda mkoani humo na
kuwekeza kwani hivi sasa kuna umeme wa uhakika.
Aidha Waziri Mkuu aliwaasa wananchi kuwa
walizni wa miundombinu ya umeme, na kuwataka wanapoona vitendo vya watu
wakihujumu mkiundombinu basi taarifa za kuwashughulikia watu hao ni vema
zikatolewa kwa vyombo husika ili kuchukua hatua.
“Naomba vifaa vyote vinavyoletwa kwenye maeneo
yenu, kwenye vijiji vyenu basi tuvilinde ili hatimaye tuweze kunufaika na
uimarishwaji wa miundombinu ya umeme.” Aliasa Wazir Mkuu.
Kupitia mpango w REA, yaani umeme vijijini
Serikali imepunguza kutoka Shilingi 380,000/= hadi shilingi 27,000/= tu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,(katikati) na viongozi wengine wa serikali wakiwemo mawaziri akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kuunganishwa umeme wa Gridi ya Taifa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika Mkoani Lindi leo Mei 21, 2018.
Waziri Mkuu Majaliwa akimpongeza Waziri Dkt. Kalemani.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, (wapili kulia), akiwa na viongozi wengine, wakiimba wimbo wa taifa baada ya kufanya uzinduzi.
Waziri Mkuu Majaliwa, na viongozi wengine, akipatiwa maelezo ya ,mradi huo na mmoja wa wataalamu wa TANESCO, kwenye kituo cha Mahumbika.
Waziri Mkuu Majaliwa, akitoa hotuba yake |
Waziri Mkuu Majaliwa, akitoa hotuba yake
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akitoa hotuba yake
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, akitoa maelezo ya mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, akitoa hotuba yake
Waziri Dkt. Kalemani, (katikati), akisindikizwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.