Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi amesema miradi ya TEDAP imeboresha hali ya umeme katika Mikoa mitatu ya Dar ea Salaam, Arusha na Kilimanjaro.
Aliongeza, Bodi imeshafanya ziara kama hiyo katika Jiji la Dar es Salaam na sasa wanamalizia katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kumepunguza tatizo la upotevu wa umeme kutokana na njia ya umeme kuwa ndefu.
Kwa upande wake Mhandisi Emmanuel Manirabona, ambaye ni Mhandisi Mkuu wa Miradi alisema miradi ya TEDAP kwa Arusha na Kilimanjaro imekamilika kwa asilimia 100 na kwa Dar es Salaam imekamilika kwa asilimia 99
Aliongeza kwa Mkoa wa Arusha mradi wa TEDAP unahusisha vituo sita ambavyo ni kituo cha Sakina, Ungalimitedi na kill Tex.
Vingine ni Njiro B, Themi na Mount Meru.
Kwa upande wake Meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha Mhandisi Gaspar Msigwa amesema mradi wa TEDAP umekuwa na manufaa makubwa katika kuimarisha hali ya umeme Mkoani wa Arusha.
Alisema, kabla ya kutekelezwa kwa mradi huo Mkoani Arusha njia za umeme zilikuwa zimezidiwa sana kwani matumizi yalikuwa makubwa kuliko uwezo wa njia hizo.
Aidha, vituo hivyo sita ambavyo vimewashwa mwezi Agosti mwaka jana, vimeonesha uwezo mkubwa wa kupunguza changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara.
" Kabla ya kukamilika kwa mradi huu Wateja walikuwa wakilalamika kupata umeme mdogo lakini kwa hivi sasa malalamiko hayo hayapo".Alisema Mhandisi Msigwa.
Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi TANESCO mbali ya kukagua mradi wa TEDAP pia ilipata fursa ya kutembelea migodi ya Mirerani na kufanya kikao na wafanyakazi wa TANESCO Mkoani Arusha .
No comments:
Post a Comment