Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt. Hamisi Mwinyimvua, amehitimisha ziara ya kikazi ya siku tatu jijini Dar es Salaam ya kukagua miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa na TANESCO kwa kuwahakikishia wakazi wa Kigamboni ifikapo katikati ya mwezi Machi, 2019, kero ya umeme itakuwa imemalizika kabisa.
Dkt. Mwinyimvua ametoa hakikisho hilo baada ya kutembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini ambacho amesema ujenzi wake umekamilika na Machi 6, kitawashwa kwa mara ya kwanza.
"Nimetembelea Kurasini ambapo ile sub station mpya kwakeli imekamilika na kilichobaki ni kuvusha nyaya kutoka Kurasini kuleta Kigamboni kazi ambayo itakuwa imekamilika ifikapo tarehe 6 Machi." Alisema na kuongeza kuwa tarehe 8 au 10 wataalamu watafanya uwashaji mitambo.
Aidha, ziara ya Dkt. Mwinyimvua alifanya ziara hadi eneo la Dege ambako TANESCO inajenga kituo cha kupoza na kusambaza umeme kwenye eneo lote la Kigamboni ambalo kwa mujibu wa Katibu Mkuu, eneo hilo linakuwa kwa kasi na hivyo Serikali kupitia TANESCO lazima ichukue tahadhari kwa kuweka miundombinu tayari ili pakitokea uhitaji huduma iweze kuwafikia wananchi bila shida yoyote.
Kwa mujibu wa Meneja wa ujenzi wa kituo cha Dege, Mhandisi Neema Mushi, kazi ya ujenzi wa kituo hicho kwa sehemun kubwa imekamilika miundombinu yake na kwamba kinachosubiriwa na kuletwa kwa mitambo ili iweze kufungwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt.Hamisi Mwinyimvua (kulia), na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, (kushoto), wakimsikilzia Meneja mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Dege, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Mhandisi Neema Mushi
Moja ya minara mirefu ya kupitisha nyaya za umeme mkubwa wenye msongo wa 132 kV kuelekea ng'ambo ya pili ya Kigamboni kutoka Kurasini jijini Dar es Salaam, zikiwa tayari na baadhi yake zikionekana kufungwa nyaya.
Mkuu wa Miradi (anayeshughulikia usafirishaji) wa TANESCO, Mhandisi Frank Mashalo(kushoto), akifafanua jambo mbele ya Dkt. Mwinyimvua, (wapili kushoto), Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, (wakwanza kulia) na Meneja Miradi wa TANESCO, Mhandisi Stephene Manda walipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam Februari 27, 2019.
Mkuu wa Miradi (anayeshughulikia usafirishaji) wa TANESCO, Mhandisi Frank Mashalo, akifafanua Zaidi kuhusu utayari wa kituo hicho.
Meneja wa Mkoa wa TANESCO Temeke, Mhandisi Jafari Mpina akieleza jambo mbele ya Dkt. Mwinyimvua.
Meneja Miradi wa TANESCO, Mhandisi Stephene Manda(kushoto), akielezea jinsi nyaya zitakavyovushwa kuelekea Kigamboni kutoka Kurasini.
Taswira ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Dege huko Kigamboni jijini Dar es Salaam kama kinavyoonekana leo Februari 27, 2019 ambapo kwa mujibu wa Meneja Mradi wa ujenzi wa kituo hicho, Mhandisi Neema Mushi, miundombinu ya kituo hicho imekamilika na kinachosubiriwa na mashine ili ziweze kufungwa.
Taswira ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Dege huko Kigamboni jijini Dar es Salaam kama kinavyoonekana leo Februari 27, 2019 ambapo kwa mujibu wa Meneja Mradi wa ujenzi wa kituo hicho, Mhandisi Neema Mushi, miundombinu ya kituo hicho imekamilika na kinachosubiriwa na mashine ili ziweze kufungwa.