Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua ametembelea Kituo cha
kufua umeme wa Gesi Asilia Kinyerezi I extension na Kinyerezi II jijini Dar es Salaam.
Lengo
la ziara yake alisema ni kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya
Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I (Kinyerezi I expansion)
Mradi
wa Kinyerezi II ambao unazalisha kiasi cha Megawati 240 tayari umekamilika na
umeme umekwishaingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
“Tunashukuru
kwamba tunaenda vizuri hasa Kinyerezi II ambayo kiukweli mradi umeshamalizika sasa
hivi tunapata umeme kilichobaki ni masuala ya kuweka kila kitu sawa baina ya
Mkandarasi na wataalamu wetu.” Alisema Dkt. Mwinyimvua baada ya kupokea taarifa
ya miradi hiyo miwili toka kwa Meneja Miradi, Mhandisi Stephene Manda.
Alisema
kwa upande wa mradi wa upanuzi Kinyerezi I, (Kinyerezi I extension) kazi
imeanza ingawa kulikuwepo na ucheleweshwaji wa vifaa bandarini na kuagiza Uongozi wa TANESCO kukutana na taasisi zinazohusika na masuala ya kodi na
utoaji mizigo bandarini ili kupanga utaratibu wa jinsi ya kulipa kodi
mbalimbali bila ya kuathiri utoaji wa mizigo hiyo (vifaa na mitambo) bandarini.
“Nakumbuka
mlipewa wito na Mheshimiwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwataka
mjitahidi isifike mwezi wa nane, ikiwezekana hata mwezi wa tano muwe mmemaliza
kazi.” Alisema.
Katika
ziara hiyo, Katibu Mkuu alifuatana na Kamishna wa Nishati kutoka Wizara ya
Nishati, Mhandisi Innocent Luoga wakati kwa upande wa Shirika la Umeme Tanzania
TANESCO, waliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Tito Mwinuka.
Akitoa
taarifa kwa Katibu Mkuu na ujumbe wake, Meneja Miradi wa TANESCO, Mhandisi
Stephene Manda, alisema wakati Mradi wa Kinyerezi II Megawati 240 ambao
umekamilika tangu Desemba mwaka jana (2018), mradi wa Kinyerezi I ambao
unafanya kazi una Megawati 150 na ule wa kufanya upanuzi (Kinyeerzi I extension)
utakuwa na Megawati 185 na kazi tayari imefikia asilimia 76%
“Tunategemea
mtambo wa kwanza wa mradi huu wa upanuzi
tutakuwa tumeuwasha ifikapo mwezi Mei, 2019 na kukamilika kabisa kwa mradi
mzima itakuwa Agosti 2019.” Alibainisha Mhandisi Manda na kuongeza Jumla ya
umeme utakaokuwa unazalishwa hapa Kinyerezi kufikia Agosti mwaka huu itakuwa
Megawati 575.” Alisema
Akifafanua
zaidi alisema kutoka pale Kinyerezi I Extension tutakuwa na extension ndogo ya kutoa umeme kwa ajili
ya mradi wa SGR.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kulia), wakiongozwa na Meneja Miradi, Mhandisi Stephene Manda (kushoto), wakati Katibu Mkuu akikagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa Gesi Kinyerezi I (Kinyerezi I expansion), jijini Dar es Salaam, Februari 25, 2019.
Katibu Mkuu pia alijionea kituo cha kupokelea gesi kikiwa tayari kwenye eneo la mradi huo. |
KATIBU
Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua, akipatiwa maelezo.
Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga(kushoto), akiwa na Mkandarasi eneo la mradi.
Katibu Mkuu Dkt. Mwinyimvua na ujumbe wake wakimsikiliza mkandarasi anayetekeleza mradi wa upanuzi Kinyerezi I, kuhusu mwenendo wa mradi huo.
Kiongozi wa zamu wa chumba cha udhibiti mitambo, kwenye mradi wa umeme wa gesi Kinyerezi II, Mhandisi Chidololo Enzi, (kulia) akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Hamisi Hassan Mwinyimvua (katikati), alipotembelea kujihakikishia kukamilika kwa mradi huo unaozalisha Megawati 240.
Kiongozi wa zamu wa chumba cha udhibiti mitambo, kwenye mradi wa umeme wa gesi Kinyerezi II, Mhandisi Chidololo Enzi, (kulia) akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Hamisi Hassan Mwinyimvua(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (wapili kushoto).
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (wapili kushoto), Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, (wakwanza kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (wapili kulia), wakiongozwa na Meneja Miradi wa Shirika hilo. Mhandisi Stephene Manda (aliyenyoosha mkono) wakati Katibu Mkuu akikagua maendeleo ya mradi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam Februari 25, 2019 ambapo alielezwa kuwa tayari umekamilika.
Hii ndiyo Kinyerezi II kama inavyoonekana Februari 25, 2019 wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Nishati, Dkt. Mwinyimvua.
No comments:
Post a Comment