January 12, 2021

Mradi wa Umeme Ruhudji, Maandalizi ya Miundombinu Wezeshi Yaanza

 

 
Maandalizi ya Miundombinu wezeshi kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Ruhudji Mw 358 yameanza rasmi.

Akiwa katika ziara ya kukagua mahitaji ya ujenzi wa miundombinu wezeshi, leo Januari 12, 2020, Kaimu Katibu Mkuu Nishati,  Mhandisi Leonard Masanja amesema mradi huo ni muhimu katika kuendeleza sekta ya Nishati ya umeme Nchini.

Ziara hiyo imefuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuanza kutekelezwa kwa miradi ya Ruhudji na Rumakali iliyopo Mkoani Njombe.

Mhandisi Masanja amesema, ujenzi wa miradi ya kufua umeme kawaida inaanza na maandalizi ya awali ambayo ni ujenzi wa miundombinu wezeshi.

"Mradi huu ni kati ya miradi muhimu, tumekuja kuanza maandalizi ya mahita ya ujenzi wa miundombinu wezeshi kama maji, umeme, barabara, na kadhalika", amesema Mhandisi Masanja.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka amesema TANESCO imejipanga kutekeleza mradi wa Ruhudji hadi kukamilika kwake.

Kazi ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme kwa maji wa Ruhudji inatarajiwa kuanza mwaka huu 2021 baada ya taratibu za manunuzi kukamilika.
 

 




 

No comments:

Post a Comment