August 15, 2017

Dkt. Kaleman amezindua REA Awamu ya Tatu Rukwa


Naibu Waziri Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akiwasili eneo la uzinduzi Mkoani Rukwa, akiwa amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mheshimiwa Saidi Mtanda.

Na Henry Kilasila, Teddy Mhagama - Rukwa



Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani ameendelea na ziara za uzinduzi wa Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA PHASE III) ambapo Agosti 14, 2017 alikuwa Mikoani Rukwa katika Kijiji cha Kabwe Wilaya ya Nkasi.

Dkt. Kalemani alisema jumla ya Shilingi Bilioni 42.5 zitatumika kupeleka umeme katika Mkoa huo na kuongeza Mradi huo utatekelezwa katika vipindi viwili tofauti ambapo sehemu ya kwanza itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 111.

"Sehemu ya pili itahusisha vijiji 145 ambapo itaanza baada ya kukamilika  kwa sehemu ya kwanza. Kufikia mwaka 2021 vijiji vyote vya Mkoa wa Rukwa vitakuwa vimepatiwa umeme".Alisema Dk. Kalemani.

Aidha, Dkt. Kalemani alimtambulisha Mkandarasi atakayejenga Mradi wa REA Mikoani humo Kampuni ya Kitanzania ya Nakuroi Investment Company Limited.

Alimwagiza Mkandarasi kuhakikisha anapeleka umeme Kijiji kwa Kijiji na Kitongoji kwa Kitongoji bila kuruka na sehemu zinazotoa huduma za Kijamii kama Mashule, Zahanati, Magereza, Visima vya maji, Nyumba za Ibada na sehemu mbalimbali.

Pia alitoa maagizo kwa TANESCO kupeleka Ofisi katika Kijiji cha Kabwe na katika maeneo yote yenye Wateja wengi lakini wapo mbali na Huduma za TANESCO.

Aliongeza kwa kuwataka Mameneja  na Watalaamu wa TANESCO kutokukaa Ofisini bali wawafuate Wateja.

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka aliwaomba Wananchi hao wa Kabwe kuwa waaminifu na kutoa ushirikiano kwa Watendaji wa TANESCO kabla na hata baada ya Mradi kukamilika.

"Muitunze Miundombinu ya umeme, msiihujumu wala kuichoma moto". Alisema Dkt. Mwinuka.

Alisema TANESCO imejipanga kuhakikisha Wananchi hao wanapata huduma ya umeme iliyobora na ya uhakika.

 Mbunge wa Nkasi, Mheshimiwa Ali Kessy  aliwaeleza Wananchi kuwa mradi huo wa usambazaji umeme vijijini hauna malipo ya fidia hivyo watoe ushirikiano kwa wakandarasi hao wakati wanatekeleza mradi huo.

Mkuu wa Wilaya ya Nkansi Mheshimiwa Saidi Mtanda aliushukuru Uongozi wa TANESCO kwa kwani umekuwa ukitoa ushirikiano pale unapohitajika.

"Mheshimiwa Mgeni Rasmi katika Kijiji cha Nyamare kwenye chanzo cha maji tulileta Mkandarasi akatukadiria bei ya Transfoma Milioni 60, tuliwasiliana na uongozi wa TANESCO wametufungia Transfoma kwa pesa zao milioni 24". Alisema Mheshimiwa Mtanda.

Mheshimiwa
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani alimalizia uzinduzi Mkoani Rukwa kwa kuwakabidhi Wazee kumi zawadi ya kifaa cha UMETA.

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCo, Dkt. Tito E. Mwinuka akiwasalimia Wananchi katika uzinduzi huo


 ,Dkt Medard Kalemani akifurahia baada ya kuzindua mradi wa REA RUKWA

Dkt Medard Kalemani akipata maelezo ya namna kifaa cha UMETA kinavyofanya kazi kutoka kwa Bw. Lucas Kusare Afisa Huduma kwa Wateja Mkoa wa Rukwa 


Kutoka kushoto Mkurugenzi Mkuu REA, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. TITO E. Mwinuka katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya Nakuro Investment Company Limited inayojenga Mradi huo wa umeme Mkoani humo.













June 28, 2017

MOTO WAATHIRI MIUNDOMBINU YA UMEME MKOANI RUKWA



NA MWANDISHI WETU
WATU wasiojulikana wamechoma msitu wa Kirando wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ambao umeunguza miundombinu ya umeme ya Shirika la umeme Nchini TANESCO.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni hii Juni 24, 2017 na Kaimu Meneja Uhusinao wa TANESCO makao Makuu, Bi. Leila Muhaji, imesema, uharibifu huo mkubwa wa miundombinu umeathiri upatikanaji wa umeme kwa wateja wa maeneo ya Kirando na Kipili wanaopata huduma ya umeme ya njia ya msongo mkubwa wa umeme unaopita kwenye maeneo hayo.
“Mafundi wa TANESCO waliofika kwenye eneo hilo, wameshuhudia uharibifu mkubwa ambapo miundombinu ya umeme imeungua na kusababisha hasara kubwa.” Alisema Bi Leila katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Bi Leila amesema TANESCO inawaomba wananchi wote waishio kwenye maeneo hayo kutoa taarifa kwenye ofisi za TANESCO au kituo cha polisi kilicho karibu ili kuokoa miundombinu ya umeme kwa manufaa ya taifa.
Amesema, tayari vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na TANESCO wameanza msako ili kuwabaini wahusika ili sheria ichukue mondo wake.

 Afisa wa polisi akiwa eneo la tukio huku akishuhudia jinsi moto huo ulivyoathiri nguzo za umeme

MOTO WAATHIRI MIUNDOMBINU YA UMEME MKOANI RUKWAMOTO WAATHIRI MIUNDOMBINU YA UMEME MKOANI RUKWA

June 18, 2017

Dkt. Mwinuka: Mradi wa umeme wa Gesi asilia aa Kinyerezi II unaendelea kwa kasi


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka (katikati), akiongozana na  Meneja wa mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, Mhandisi   Simon Jilima,(kushoto) na Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere, wakitembelea kukagua maendeleao ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, leo Juni 17, 2017.

NA Grace Kisyombe
SHIRIKA la Umeme Nchini, (TANESCO), limewahakikishia Watanzania kuwa mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II unaendelea kwa kasi kubwa na utakamilika kama ilivyopangwa.

Hakikisho hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka, wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam, ambao unatarajiwa kutoa Megawati 240 za umeme.
“Niwahakikishie watanzania kuwa ifikapo Agosti mwakani (2018), mradi wa umeme Kinyerezi II utakamilika na hivyo tutaongeza Megawati 240 kwenye gridi ya Taifa.” Alisema Dkt. Mwinuka wakati akitoa majumuisho ya ziara yake.
Dkt. Mwinuka alifuatana na wakurugenzi watendaji wasaidizi, Mhandisi Abdallah O. Ikwasa, (anayeshughulikia Uzalishaji), Mhandisi Khalidi James, (anayeshughulikia uwekezaji miradi) na Mhandisi Kahitwa Bishaija (anayeshughulikia Usambazaji).
Dkt. Mwinuka alisema watanzania wanahitaji umeme ulio wa uhakika na kwamba Serikali kupitia TANESCO imejipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana kwa watanzania na hivyo kuchangia pato la taifa.

“Kama mjuavyo Serikali imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha Shirika linatekeleza miradi hii na tayari shilingi Bilioni 110 zimetolewa na serikali katika kutekeleza mradi huu wa Kinyerezi II.” Alifafanua Dkt. Mwinuka.

Awali Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Stephens S.A.Manda, alisema, wataanza kuingiza umeme kwenye gridi ya taifa kila mwezi kuanzia Desemba mwaka huu 2017 ambapo Megawati 30 zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa.

“Tuna mashine 8 ambazo zitafua umeme huo kwa hiyo kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, tutaingiza megawati 30 kwenye gridi ya taifa na tutafanya hivyo kila baada ya mwezi mmoja kwani tunaelewa kuwa serikali ambayo imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda, tunaona umeme ni hitajio muhimu kwa hivyo kila tutakapokamilisha mtambo mmoja tunaingiza umeme kwenye gridi ya taifa hatutasubiri kuwasha mitambo yote minane.” Alisema Mhandisi Manda.
Mhandisi Manda alisema, mradi mzima ambao umeanza kutekelezwa rasmi Machi 3, 2016, utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 344,059,746.00 kati ya hizo asilimia 15 zimetolewa na serikali.

“ Kufikia leo Juni 17, 2017, asilimia 63 ya ujenzi wa mitambo imekamilika, na tunahakika ya kukamilisha ujenzi wa jumla kwa vile tayari mitambo yote inayohitajika imeshalipiwa na mingine iko njiani inaletwa nchini.” Alifafanua na kuongeza mitambo yote iliyoagizwa na TANESCO imo kwenye makontena 900 na tayari makontena 400 na ushee yamekwishawasili na baadhi ya mitambo imefungwa na tunatarajia mashine zingine kwenye hayo makontena yaliyosalia zitawasili nchini wakati wowote. Alisema.

Akizungumzia kuhusu makontena 20 yaliyokuwa yamezuiliwa na TRA bandarini, Mhandisi Manda alisema, taarifa hizo hazina msingi wowote kwani kiasi hicho cha makontena 20 ni sehemu ya makontena 900 na tayari TANESCO imeshalipa fedha hizo za kodi na mizigo hiyo imefika site.

Katika ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Mwinuka ;pia alitembelea mradi wa umeme wa upanuzi wa Kinyerezi II ambako nako ameridhishwa na kasi ya ujenzi wake. 
Mradi huo ambao unasimamiwa na Mhandisi Simon Jilima, utawezesha ongezeko la megawati 35 na hivyo Kinyerezin I ambayo inatoa Megawati 150 itakuwa na uwezo wa kutoa Megawati 185 za umeme.

 Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda
 Meneja wa mradi wa upanuzi Kinyerezi IMhandisi Simon Jilima
 DKT. Mwinuka, (kulia), Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James, (katikati) na Meenja Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen A.S.Manda, wakijadiliana jambo
 Mitambo ikiteremshwa eneo la ujenzi
 Mkurugenzi wa Business Times, Imma Mbuguni, (kulia) akizungumza jambo na Mhandisi, Khalid James
 Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere(kulia), akiteta jambo na Kaimu Meneja Uhisano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji
 Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme (Generation), Mhandisi Abdallah O. Ikwasa(kulia), akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere
 Mhariri Mtendaji wa Business Times, Bw. Imma Mbuguni, akizungumza ili kuoata ufafanuzi wa maswala kadhaa
 Baadhi ya mitambo ikiwa eneo la ujenzi ikisubiri kuunganishwa
 Mtandao wa nguzo za umeem ukiwa tayari kwa sehemu kubwa
 Kaimu Meenja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji akifafanua baadhi ya mambo kuhusu namna Shirika hilo linavyotekeleza sera ya kusaidia jamii (Corporate Social Responsibility), ambapo alisema, licha ya shirika imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii sio tu kwenye maeneo ambako mradi unapita bali pia maeneo mengine na kutolea mfano wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera, kamati ya kikosi kazi cha kuokoa mazingira, na hata shule. Kushoto ni Dkt. Mwinuka na Mhandisi Khalid James
 Dkt. Mwinuka akiwa amezungukwa na wasidizi wake akizungumza kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II
 Dkt. Mwinuka (kulia), akiongozana na wakandarasi toka kampuni ya kijapani SUMITOMO amabao ndio wanajenga mradi huo
Dkt. Mwinuka (kushoto), Mhandisi Ikwasa(katikati) na Mhandisi Chegere