November 30, 2010

RATIBA YA MGAO WA UMEME KWA BAADHI YA MIKOA

Ndugu wateja, Unaweza kubofya katika jina la mkoa husika hapo chini kupata ratiba ya mgao wa umeme kwa baadhi ya mikoa:-

Tunawasihi wateja wetu na wananchi kwa ujumla kuwa na subira wakati jitihada zinafanywa kukabiliana na mgawo huo wa dharura

20 comments:

  1. Tanesco - welcome to the world. I wonder why there's no K'ndoni North in the list above au hakuna mgao au ndo wanakaa wakubwa - kwa hiyo hawakatiwi.

    ReplyDelete
  2. Mpendwa Badra, pongezi nyingi but i hope you understand the impact of having a tool like this (blog) and not using in effectively. i believe you'll have a person dedicating in dispatching our comments to the right people/dept ASAP

    ReplyDelete
  3. Hi,
    Mimi naomba nitoke nje kidogo ya mada ya mgawo wa umeme. Mimi ni mteja wa TANESCO nilikuwa nikilipa umeme wa bill miaka iliyopita mpaka nilipofungiwa LUKU mwezi wa tano mwaka huu na nilikuwa mlipaji mzuri sana kila mwezi bila kulimbikiza. Chakushangaza baada ya miezi mitatu baada yakuwekewa LUKU nilinunua LUKU kama kawaida nakukatwa nusu ya hela niliyonunulia na chini ya risiti lilionyeshwa deni la 96,000/=! Niliendelea kukatwa nusu ya hela kila niliponunua umeme. Ilinilazimu niende TANESCO Ilala ili kujua kulikoni baada yakuonyesha risiti zote mpaka ya mwezi wa nne niliyolipia umeme wa bill, niliambiwa baada ya kuwekewa LUKU bill ilikuwa inasoma kama kawaida hivyo deni lilikua linaingia kama kawaida licha ya kununua LUKU! Nilishauriwa niende kwa mhasibu ili asitishe bill na kuangalia uwezekano wakurudishiwa hela nilizokatwa. Mpendwa Bi Badra hadi ninavyoandika hii comment sijafanikiwa kumuona huyo mhasibu kila nikienda mara hakuna network mara ametoka! Naendelea kuumia na wala sijui hatma ni nini!

    Naomba kujua nitapataje haki yangu, kwa sababu ukweli sina deni na hata wahusika walithibitisha kwa kuona risiti zangu, how comes naletewa deni from no where!

    Natumaini nitapewa muongozo wa jinsi yakupata haki yangu kwa kupitia blog hii.

    Wako

    Mteja mwaminifu.

    ReplyDelete
  4. Ndugu mteja uliyetoa pongezi...Asante sana na tunapenda kukufahamisha kuwa maafisa wetu wanaotoa huduma kwa wateja kwa kila mkoa husika Tanzania Nzima watakuwa wanayajibu maswali yenu na kuwasaidia moja kwa moja..

    Ndugu mteja mwenye tatizo kutoka TANESCO Ilala..tunaomba ututumie jina kamili na namba yako ya simu kupitia info@tanesco.co.tz ili tuweze kukupa majibu ya tatizo hilo ulilolipata..Pole sana na tutakupa jibu kupitia namba ya simu utakayotutumia..Asante

    ReplyDelete
  5. nyie watu vipi kwani mmesikia Badra ndio atakuwa anajibu kwenye blog hii, hapo ndio eneo lingine ambal tunafikiri mawazo yetu yatakuwa kichekesho. maana hatujua hata tunamuaddress nani. wekeni mtu special wa kudeal na blog ili kama akiminyia comments tunamchana live.

    ReplyDelete
  6. Hi all,Kwanza kabisa nawapa pongezi sana kwa kuanzisha hiki chombo cha mawasiliano.Ni ubunifu mzuri. Naomba nianze kuwakilisha mada yangu. Mimi nakaa uswazi kidogo maeneo ya Flat za Tazara. Mgao wa umeme najua kwamba upo na nimeukubali kwani matatizo huwa yapo. Tatizo lililopo ni fairness katika ugawaji!Sehemu niliyopo tunapata umeme masaa nane tu. Kuanzia saa 8mchana mpaka saa 4 usiku. Cha kuhudhunisha ni kwamba maeneo jirani to pale chang'ombe wanapata 16hrs. Mbaya zaidi hiyo ratiba iko very fixed. At least tungegawana hayo masaa na iwe ina rotate.

    ReplyDelete
  7. Mgawo, mgawo, mgawoooooooooo, shame on you.

    ReplyDelete
  8. Mimi nawapongeza kwa kuanzisha Blog hii kwa kweli tutapata pa kuweka machungu yetu. Kwa upande wa Iringa hawa jamaa wanaosoma mita hawapiti kusoma mita wakati mwingine, na kusababisha bill inayokuja isioane na kiasi cha umeme uliotumika kwenye mita mwezi huo.

    Niwaombe muwahimize wapite hasa yale maeneo ambayo hamjafunga LUKU. Kwa kweli inaboa sana, wakati mwingine tunashindwa kuleta malalamiko ofisin kwa kuwa na sisi tunakuwa kazini kama nyie.

    ReplyDelete
  9. Haya Tanesco tunaanza kama ifuatavyo,kuna makazi mapya kule kajiungeni(karibu na kipawa mpya) plz anzeni kufkiria kufikisha japo nguzo kadhaa barabarani watu wapate huo umeme japo wa mgao lakini wawe nao coz kule seems hakuwekwi leo au kesho,japo watu wachache ila nguzo zikifika ofcoz hata hao ambao hawana mpango wa kujenga watawaza cha kufanya as well.
    Kingine watu wafanye kazi kwa uchungu wa nchi na si kwa how much wanapata,tunawaomba kila mtu hapo kazini akiambiwa hivyo japo kichwa maji lakini mwisho ujumbe utamfikia tu!Hapa hapakuwa kwa kucomment hii ila sikuona pengine labda kuwepo mahala pa kutoa comment km hizi!
    Kazi njema!

    ReplyDelete
  10. Leo ni Alhamisi wtu wa Tandale hatumo kwemye mgao mbona mmekata kuanzia saa tatu asubuhi?

    ReplyDelete
  11. ...yaani basi 2 ndio ishakuwa ivyo, ila mnavyokera ni Mungu pekee ndio anajua

    ReplyDelete
  12. Kero kubwa ni hiyo habari ya mgao.
    Wananchi hatutaki kusikia kabisaaaaa.
    Jaribu kutafakari wenyewe, mishahara, matengenezo ya samani na mali, kodi za viwanja, kupanua huduma, zote mnahitaji pesa, chanzo kikuu cha pesa ni malipo ya bili halali za wateja. Kama mnaendelea na mgao huo, mtaweza kweli kujiendesha.
    Nawashauri muanze na mgao wa mishahara ya wafanyakazi wenu kupunguza hasara manayoipata kila siku kuliko kuleta mada ya kupandisha gharama za umeme huku hapunguzi matumizi yasiyo na tija.
    Tupeni umeme kila siku muone kama mtapata hasara tena. Tanesco tunawataka mgeuke na muangalie njia mbadala ya kuendesha shirika kwa ufanisi.
    Wanaojaribu kulitia hasara shirika kutoka ndani na nje muwaadhibu kabisa.
    Nawatakia kila la heri

    ReplyDelete
  13. kama mtakua mnayafanyia kazi haya maoni mnaweza kurekebika ila sijui kwani tanesco wana kiburi wapo wenyewe hakuna mpinzani. mimi naishi tabata kisukulu kama unaenda makoka kanisani tatizo kila siku kule kuna mgao wa umeme kipindi cha mvua nadhani mvua inakua nyingi lazima wakate, sasa kipindi cha jua tumesikia maji yamepungua mgao unaendelea. wakati jirani kinondoni kila unapokatika kwetu kwao unawaka bila tabu. wiki kama ya pili sasa umeme unakua mdogo kiasi cha kwamba hata taa ya energy save inawaka kwa kufifia sana na hiyo ni kila siku nafikiri tatizo hili mnalijua kama hamlijuia nimewaarifu na mlifanyie kazi, natumai nitapatiwa jibu kupitia hii forum kama kweli inafanya kazi na imewekwa kwa ajili ya kukuza na kuboresha shirika. maana imefika mahali tunasali lizaliwe shirika m badala kwa mambo yenu, please answer me

    ReplyDelete
  14. awali ya yote nakupongezeni sana kwa kuanzishwa kwa blog hii...
    pili naombeni habari ya blog isiwe mbio za sakafuni. lakini pia isiwe kelele za mpangaji zisizomnyima mwenye nyumba usingizi wake.........
    jambo jingine jamani Tanesco hebu boresheni mfumo wenu wa utoaji wa huduma.....wananchi wengi inafikia pahala twaona kama si mali yetu hili shirika........naamini hata ukifanya utafiti utagundua watu wengi hukatishwa tamaa na kata kata ya umeme ambayo daima hutuachia maumivu ya kuunguliwa na vifaa vyetu....
    walahi vile siwezi isahau Mei 16, 2008 majira ya jioni nilipounguliwa na vifaa vyangu vyote vya umeme nyumbani kwangu...kisa mnajua kilikuwa nini? niliwasili nyumbani panapo saa kumi na moja na kuwasha vifaa vya umeme ikiwemo radio na runinga....wakati nataka kuketi umeme ukakatika...nageuza nirudi kuzima soketi ukutani, umeme ukarudi kwa nguvu na kuunguza vifaa vyangu...aisee hebu wacheni jamani mnatuumiza sana....
    sasa hivi hakya kweli naijua hata bei ya mafuta ya taa na mishumaa kwani ile kauli mbiu yenu ya zamani (ishakuwa ya zamani sana) "Maisha ni rahisi ukitumia umeme" naona haina thamani tena...
    maji hatuyapati kwa kuwa mgao wenu unafanya mashine za kusukuma maji zisifanye kazi kabisa....
    ngoja leo nikomee hapa, lakini Tanesco jirekebisheni kwa kweli.

    ReplyDelete
  15. Tanesco, kwakweli mna maudhi mengi sana yaani sana, may be kwa sababu ya monopolism. but angalia haya baadhi tu.
    1. Kuwepo kwa Mgao ni kwa sababu ya baadhi ya watendaji wamezembea kwenye majukumu yao. na pia poor planning, management haiwezi hata kupanga back up plans. mpaka litokee jambo ndio mnakimbilia kwenye mgao. Achaneni na kawaida kuweni wabunifu wa kutatua matatizo.
    2. Kupata umeme Tanesco ni isue ambayo watu wakimalizan nayo wanaenda kuinywea bia kupoza machungu. Unaweza kuapply umeme leo ukaupata baada ya miezi mitatu tena kwa kuwahonga baadhi ya watu, especially mafundi, engineers na watu wa stores ili kupata vifaa. this is the sign of kutokuwajibika jichunguzeni wenyewe mtu akibaii kuleta zake usmfukuze kazi mwache akae ofisin tu bila kuwa assigned any duty.

    3. Nguzo tunalipia bei kubwa sana, mananchi wa kawaida atapata wapi 900,000 kwa nguzo moja? lakini cha ajabu ukivuta umeme hata kama umegharimia kiasi gani, mwenzako akitaka kuvuta umeme ankuja kwenye nguzo uliyo nunua kwa pesa nyingi, bila kukufidia chochote.

    ReplyDelete
  16. Bwana Fadhili Mtanga, ndio maana Insurance zipo. yaani na ukubwa huo hujajua maana ya kuchukua insurance ya vitu vyako au nyumba yako? acha hizo braza.

    ReplyDelete
  17. We Annony hapo juu, hivi unajua kwa kipato cha kawaida cha Mtanzania kumwambia mtu aweke bima ya vifaa vinavyotumia umeme ni sawa na kumtusi...
    hata wewe acha hizo Bro!

    ReplyDelete
  18. We never have power for the last month from 10.00 a.m. till 7.00p.m. if u call tanesco they zarrow u they dont answer if the call the manager he is always in meetings could u tell us wat is happening we are located at Jamhuri and Zanaki St, is this power rationing or wat because as we are the customers of tanesco and we would like to know why we dont get power and everyone else in the block on the other side has power. Plse do the needful on this matter.

    ReplyDelete
  19. jamani hivi nyie tanesco mna matatizo gani kwani kila mara matatizo mnayo nyie tu kabla ya ya uchaguzi tulikuwa tuna umeme kila siku na hakuna tatizo lolote ila baada ya uchaguzi ndo yanatokea haya/ kwa hiyo mna maana malikuwa mnataka tuwape kwanza kura ili mtufanyie haya? kwa kweli tumechoshwa na hali hii kwani ina athiri uchumi mara umeme mara maji hakuna sasa tutaishi vipi

    ReplyDelete