March 10, 2011

Wanawake wakiwezeshwa wanaweza


Leo ni siku ya wanawake Duniani, ambapo watanzania wote tunaungana na wanawake kote duniani kusherehekea miaka 100 ya tangu kuanzishwa kwa siku hiyo.

Licha ya changamoto nyingi ambazo wanawake wamekuwa wanakutana nazo sehemu za kazi, majumbani na ndani ya jamii kwa ujumla, Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limekuwa mstari wa mbele katika kulinda haki na usawa kwa jinsia zote.

TANESCO ni Shirika linalofanyakazi zake za msingi zenye asili ya kiuhandisi yaani uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme. Hadi kufikia Januari 2011, Shirika lilikuwa na jumla ya wafanyakazi 5736, ambapo kati ya hao 1148 ni wanawake na 4588 ni wanaume.

Kwa upande wa uongozi, wapo wanawake wanaoshikilia nafasi za juu za uongozi na wanafanya vizuri. Baadhi ya wanawake hao ni Meneja wa Kanda ya Ziwa Bi.Joyce Ngahyoma, Afisa Mkuu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Bi.Salome Nkondola na Meneja Mwandamizi Rasilimali Watu Bi.Victoria Elangwa.

Wengine ni Meneja Mwandamizi Usambazaji Umeme Bi.Sophia Mgonja, Meneja Mwandamizi Hesabu za Fedha Bi.Anetha Chengula, Kaimu Mkaguzi Mkuu Hesabu za Ndani za Shirika Bi.Zelia Nyeza na Katibu wa Shirika Bi.Subira Wandiba.

Wapo pia Mameneja wa wanaotawala mikoa, Mameneja wanaoongoza vitengo mbalimbali ofisi za Makao Makao makuu na Mameneja wa wanaoongoza wilaya.

Baadhi ya Mameneja wanawake wanaoongoza wilaya ni Meneja wa Wilaya ya Mafinga Bi.Esther Ngailo, Meneja wa Wilaya ya Mbarali Bi.Joyce Shimba, Meneja wa Wilaya ya Handeni Bi.Cecilia Lyimo, Meneja wa Wilaya ya Kateshi Bi.Marietha Chimwenda na Meneja wa Wilaya ya USA-River Bi.Harriet Kimerei.

Wengine ni pamoja na Meneja wa Wilaya ya Kiteto Bi.Elioza Kachira, Meneja wa Wilaya ya Tukuyu Bi.Ludia Kiangi na Meneja wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Sarah Assey.

Ukiacha wanawake hao wenye nafasi za uongozi ndani ya Shirika, TANESCO pia inajivunia idadi kubwa ya wafanyakazi wanawake wenye fani na ujuzi mbalimbali ambao wameonyesha uwezo kuwa wakiwezeshwa kwa kupewa nafasi mbalimbali wanaweza.

1 comment:

  1. Orodha hii ya wanawake watendaji ndani ya TANESCO ni changamoto kwa asasi zote za serikali na zisizo za kiserikali katika kutimiza ile kauli mbiu:"WANAWAKE WANAWEZA".
    Wakati hayo yakiendelea huko TANESCO,wanawake wa eneo la Kitunda Mzinga-Tsunami(Kwa mzee Njovu) wamevunja ukimya na kumuomba diwani awasilishe kilio chao cha muda mrefu kwa meneja wa TANESCO wilaya ya Gongo la Mboto.Kilio cha ni kuendelea katika miradi ya ujenzi wa laini za nishati ya umeme.Kila kukicha laini zinajengwa lakini eneo la kwa mzee mzee Njovu limegeuka kisiwa.Kisima kilichopo hapa kimegeuka makumbusho baada ya jenereta kuharibika.Wanawake ndiyo waathirika nambari moja wa tatizo hili.Wanawake wenzao wa TANESCO watawawezeshaje wanawake wenzao wa KITUNDA MZINGA -TSUNAMI [KWA MZEE NJOVU] ili waunganishwe kwenye mradi mpya wa laini ya umeme kutoka eneo la MADAWA kupitia UZUNGUNI?

    ReplyDelete