March 16, 2011

KITUO CHA KUTOA HUDUMA KWA WATEJA KWA NJIA YA SIMU CHA TANESCO (TANESCO CALL CENTRE)

Taarifa kwa umma


SIMU: 2 19 44 00

Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO, linapenda kuwajulisha wateja wake kuwa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Wateja cha TANESCO kimeanza kutoa huduma kwa wateja  tangu Machi 16, 2011 kwa saa 24.

Huduma imeanza kutolewa kwa wateja wa Dar-es-Salaam na Kibaha tu. Kwa kuanzia Kituo kimeanza kupokea na kujibu simu za wateja kwa ajili ya huduma zifuatazo:

  1. 1.     Matatizo ya umeme ya dharura.
  2. 2.     Taarifa na msaada kuhusiana na huduma mbalimbali za kununua LUKU kama vile ZAP, MPESA, Mobile, NMB, ATM na MAXMALIPO.
  3. 3.     Taarifa na ufafanuzi kuhusu maombi ya kuunganishiwa umeme.


Ili kupata mojawapo ya huduma zilizotajwa hapo juu, wasiliana nasi kwa simu nambari  219 44 00. Wahudumu wachangamfu na wenye ari watakuhudumia kwa haraka na uhakika.

“TANESCO Tunayaangaza Maisha yako”

84 comments:

  1. namba hiyo ni kwa matumizi ya wakazi wa jiji tu ama hata mikoani?
    Kuna haja na uharaka wa kulimulika desk la dharura hapa tanesco moshi mjini maana uzembe wa kuto kupokea simu utaigharimu tanesco siku za karibuni. Japo suala hili kwa sasa ni mzaha lakini linahitaji uangalifu. Umeme umekatika maeneo ya rau tangu saa saba usiku . Jitihada zote za kuwafikishia taarifa zimekwama kwakuwa hawapokei simu. Nimeamka saa mija asubuhi na kujaribu kupiga tena bado sipati jibu kwakuwa simu haipokelewi. Nimeendesha gari hadi nje ya ofisi na kiko nje ya dirisha la dharura ninapiga simu yangu ya mkononi kwenda land line ya tanesco inaita na mtoa huduma yupo anaisikia na anasoma gazeti la udaku as if haoni wala kusikia simu hiyo. sasa hapo tunaitaje? Ndio umulikaji wa maisha yetu???????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona namba yenu haipatikani, huku maeneo ya mhezi makabe kuna maeneo hayana umeme tangia jana tatizo ni nini??

      Delete
  2. Ujumbe huu tumesha ufanyia kazi, na tatizo lililokuwepo ni kuwa siku ya Ijumaa, watu wa TTCL walikuwa wanafanya matengenezo katika mifumo(underground cables ) yao iliyo hapa katika eneo la ofisi(nje ya ofisi ya mkoa ). kutokana ma natengenezo hayo mfumo mzima wa simu za ndani ya jengo la Tanesco mkoa ulikuwa umepata hitilafu hivyo kufanya mawasiliano ya ndani na yale ya nje kuto kupatikana kabisa, yaani simu zikipigwa toka nje . inakuwa inaita lakini ukipokea kunakuwa hakuna mawasiliano yoyote na simu inaweza ikaendelea kuita kana kwamba haijapokelewa,
    Kwa bahati mteja huyu aliweza kufika katika ofisi ya mkoa na kutoa lalamiko lake na pia kujaribu kuipiga simu ya dharura akiwa hapo ofisini na kujionea mwenyewe tatizo lililo kuwepo, na japo hakuridhika na maelezo, siku hiyo hiyo (JUMAPILI) mnamo majira ya saa nne usiku , mteja huyu aliwasiliana na mimi, kwa kupitia simu ya mkononi yenye namba 0715417152 (LOUIS KIFANGA ) na kunielezea tatizo lililo tokea , kwa muda huo pia tuliweza kumpatia huduma kama kawaida , na pia niliweza kumuelezea tatizo la simu zetu. japo kuwa alikuwa amesha andika ujumbe huo katika mtandao.
    Kwa maelezo hayo napenda kukufahamisha kuwa matatizo ya mteja huyu yalisha shughulikiwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Helloo,
      Nimelipia umeme as per details here below na mpaka sasa sijapata talken amount please do the needful.

      4F78NT1BCC Imethibitishwa. Tsh25,000.00 imetumwa kwa LUKU2-TANESCO kwenye akaunti namba 43001454644 tarehe 7/6/17 saa 11:32 AM. salio lako la M-Pesa ni Tsh15,004.73.

      Delete
  3. Hii huduma njema sana lakini ni vema watoa huduma mahiri na makini katika tasnia ya habari na mawasiliano kwa umma.Wadau wanahitaji huduma ifaayo kwa wakati ufaao.
    Wakati hayo yakiendelea sisi wadau wa Kitunda Mzinga-Tsunami[Kwa Mzee Njovu] tunasubiri kwa hamu sana kuunganishwa katika mradi mpya wa nishati ya umeme unaotokea eneo la Madawa kwenda Uzunguni.Nishati hii ni muhimu sana katika eneo letu kwa ajili ya kisima cha maji ambacho huduma yake inazidi kudorora kutokana na ubovu wa jenereta.

    ReplyDelete
  4. "HUDUMA HII NI NJEMA SANA LAKINI NI VEMA WATOA HUDUMA WAKE WAWE MAHIRI NA MAKINI KATIKA TASNIA YA HABARI NA MAWASILIANO KWA UMMA ILI KUKIDHI KIU YA WADAU WA TANESCO"

    ReplyDelete
  5. VIPI MBONA NIMENUNUA UMEME KWA NJIA YA NMB MOBILE ILA TANGU SAA MBILI USIKU HADI SASA SIJAPATA MESSAGE YA UMEME NA FEDHA IMEKATWA?

    ReplyDelete
  6. Pole sana kwa usumbufu ulioupata..Tunaomba wakati unatuma "comment" yoyote kuelezea tatizo ambalo lahitaji "feedback" kutoka kwetu uache na mawasiliano ya jinsi tutakavyoweza kukupata..aidha email au namba ya simu..ila kama ni shida ya haraka sana tunaomba uache namba ya simu...Asante

    ReplyDelete
  7. jamani tunateseka n kukatiwa umeme kwa mda w masaa kuanzia kumi mpaka kumi n nane n kurudishiwa masaa manne halafu kukatiwa tena usiku wa manane mpaka asubuh.tunashindwa kulala kwa joto n mbu kwa kuacha milango wazi.watoto wanalizana hatimae asubuh wanashindwa kwenda mashuleni kwa kuchoka n sisi wazazi tunachelewa kwenda makazini au hata kuchelewa n wakati mwingine kushindwa kufanya kazi vyema kwa machofu! sasa huku ni kuangaziwa maisha au kutiliwa giza maisha!!!tunaomba msaada.mimi mkazi w magomeni mwembechai

    ReplyDelete
  8. Nasikitika sana sijafungiwa umeme zaidi ya wiki mbili nguzo zimechimbiwa. umeme mpaka leo sijaunganishiwa sielewi kwanini na watu wenu wanapita hapo walipokuja walisema tukate mti ili umeme uwekwe tumekata mti na tukawapa taarifa wakasema watakuja mpaka leo nasikitika sana hawajafunga wanasema waya hakuna sasa wamesimamisha miti ya nini ndio huduma hiyo kweli napatikana kibada kigamboni 0767347799 au 0655347790

    ReplyDelete
  9. Hii ni taarifa maridhawa kwa watumiaji wa umeme.Je mtoa taarifa atapata tozo la kutumia hii namba?

    Ray E.Njau
    Balozi wa Tanesco
    Gongo la Mboto

    ReplyDelete
  10. Huku songea kuna tatizo gani mtaa was kwa gassa baadhi ya nyumba hazina umeme na namba ya dharula haipatikani na LA kushangaza zaidi yaani jirani yaki Ana umeme wewe hauna na ni kwa nyumba nyingi sasa namba haipatikani tunatoaje taarifaa wengine tunategemea umeme kuhifadhi bidhaa na vyakula tunaombamuweke na namba za simu za mkononi ili tywapate pale tunapokuwa nashida nanyi

    ReplyDelete
  11. Umeme umekatika ingawa luku INA units za kutosha. Majirani wana umeme isipokuwa nyumba hii tu 32 Silvester Street, Sinza E, DSM. Screen ya luku inawaka na kuzima. Tatizo limeanza tangu SAA 12:30 hivi Leo asubuhi. Tunaomba msaada Wa haraka tafadhali. Dr Jaffar, 0718195041, kwa Mama Amina Mohammed, Jirani kwa Mwaibula

    ReplyDelete
  12. Nimenunua Umeme, Lakin batani za mita hazitaki kupokea. Ttzo ni nini


    Malipo yamekamilika.43001181619
    Rcpt MAXCO33EMDB03987247
    Units 70.2KWH

    Token 0657 1104 8930 6214 3197

    Cost TZS 20491.81
    Serv Charge TZS 0.00
    Tax TZS 4508.19
    Total TZS 25000
    eSign 01/01/17 19:30


    0656560640

    ReplyDelete
  13. Tanesco makao makuu tafadhali ongezeni ofisi au kituo cha kutoa huduma kwa eneo la chanika.Kisarawe wamezidiwa au wanafanya kazi kwa mazoea kisingizio wana hudumia eneo kubwa sana.Kila idara au kitengo kimezidiwa mpaka meneja mwenyewe anatoa majibu ya kawaida tu kama hakuna umuhimu wa hiyo ofisi.kama watu wamebadilishwa sana ila bado kuna uzembe wa maksudi katika utekelezaji wa kazi.
    Kwa kweli Tanesco Kisarawe imekubuhu kwa kutoa huduma mbovu na hakuna mabadiliko yoyote sababu wanajua mteja anajileta mwenyewe.Tanesco Tanesco Kisarawe badilikeni kwani mnavyotoa huduma mbovu leo kesho kwa kizazi chenu pia.Tunaomba kitengo cha huduma kwa wateja makao makuu Tanesco waje wenyewe kusimamia maombi yote yaliyowekwa kando kwa sababu binafsi yashughulikiwe haraka iwezekanavyo.

    ReplyDelete
  14. Umeme hapa Mbweni Block 2 Mageti mawili hauna nguvu. Unawaka dim dim tangu mchana. Dr. Sokile 0754210701

    ReplyDelete
  15. Tanesco mimi chanika juzi umeme umekatika kwangu kurudi kwingine unawaka kwangu hauwaki wala kwenye meter hausomi nimepiga simu mpaka leo wanasema wanakuja hawaji 0763819541

    ReplyDelete
  16. Nakaa nyumba ya kupanga ambayo tayari ina umeme napenda kujua gharama za kufunga separate meter niwe natumia peke yangu

    ReplyDelete
  17. Line ya umeme karanga moshi mtaa Wa sambalai unakatwa kila siku saa moja jioni kurud saa Tisa kesho yake tatizo hatujui ni nn? Mana raha ya umeme usiku sasa usiku ndio wanakata kila siku

    ReplyDelete
  18. Nimenunua umeme kupitia max malipo tumeweka Zaidi ya Mara mbili umegoma nimenunua kwa wakala mwingine pia umeme umegoma kuingia nifanye nini naomba ushauri nipo gizani kwa sasa.nipo dsm 0756868910

    ReplyDelete
  19. Nimenunua umeme kupitia max malipo tumeweka Zaidi ya Mara mbili umegoma nimenunua kwa wakala mwingine pia umeme umegoma kuingia nifanye nini naomba ushauri nipo gizani kwa sasa.nipo dsm 0756868910

    ReplyDelete
  20. Jamani nimenunua luku mpaka sasa sms haijarudi na hela mmekata naombeni msaada maana wapangaji hawanielewi... 0654434165 namba yangu hiyo nisaidieni kwa haraka jamani

    ReplyDelete
  21. Tanesco mnisaidie nimelipia kufungiwa umeme toka oct 2016 nahitajika nguzo 2 niko mwanza nyegezi nahudumiwa na tanesco mkolani sasa ni zaidi ya miezi 6 nakaa gizani mlipokea hela ya nn kama hamna hizo nguzo vifaa vyangu vya umeme vinaharibika nimelalamika sana kwenye facebook page yenu naona mmenichoka naombeni mnijibu tu napata lini umeme namba yangu ni 0713857874 au 0762171715

    ReplyDelete
  22. Malipo yamekamilika.22124254032
    Rcpt MAXCO33EMDB42680595
    Units 25.3KWH

    Token 4824 7411 8294 5945 5439

    Cost TZS 7377.05
    Serv Charge TZS 0.00
    Tax TZS 1622.95
    Total TZS 9000
    eSign 22/05/17 22:35

    Mimenunua umeme jana na token nimepewa na uhakika sija kosea namba za meter lakini hizi token hata ujaze vipi umeme hauji na tumelala giza jana. Nimeqasiliana na tigo nilipo nunua umeme waka nipa namba za kuwasiliana na nyie ambazo ni 0678985100 namba hii kwa bahati mbaya imefungiwa...tafadhali mnisaidie hizo token kama sio zenyewe nipeni zingine

    ReplyDelete
  23. Habari umeme kwangu umeisha nimenunua ila hii remot ya kuweka umeme kila nikiweka inaandika connect bila ya majibu naomba msaada wenu .0789850422

    ReplyDelete
  24. hello, msaada tafadhali nimenunua umeme jana usiku saa 4:04am mpaka sasa sijapata token. Meter namba ni 01311209090, code ya MPESA ni 4FS0P6E154.
    Naomba unitumie token tafadhali.
    Dr. Swai

    ReplyDelete
  25. Habari!Tawi la Kisarawe,Pwani,hudumieni wateja kama mnavyojinadi(sabasaba July 2017):0710530083

    ReplyDelete
  26. Umeme umekatika Kinondini nzima. Tatizo ni nini? Je utawahi kurudi? Ahsante

    ReplyDelete
  27. Malipo yamekamilika.24217763481
    Rcpt MAXCO33EMDB63841385
    Units 9.9KWH

    Token 3031 4109 0580 5623 4826

    Cost TZS 2868.86
    Serv Charge TZS 0.00
    Tax TZS 4131.14
    Total TZS 7000
    eSign 03/08/17 21:28 ni sahihi kweli? Mbona sijaelewa?

    ReplyDelete
  28. Nimenunua Luku
    Lakini nikiingiza number naambiwa Zimetumika (Used) nikanunua tena bado tatizo Hilo

    Tena kwa mtandao tofauti bado haziingii nini shida?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari, ulifanyaje kuhusu token ulivyoambiwa 'used'? Ulipata msaada wowote toka tanesco

      Delete
  29. Habari

    Nimenunua through mobile lk sasa ni kama lisaa na nusu sijapokea message ya token.

    Naomba msaada wenu urgently.

    0758939566.

    ReplyDelete
  30. Habari,

    Nimenunua umeme kupitia Mpesa naambiwa "used"
    22118076177
    Rcpt MAXCO33EMDB66576155
    Units 14.1KWH

    Token 5415 9322 5825 7106 3254

    Cost TZS 4098.37
    Serv Charge TZS 0.00
    Tax TZS 901.63
    Total TZS 5000
    eSign

    Msaada

    ReplyDelete
  31. Habari,

    Nimenunua umeme kupitia Mpesa naambiwa "used"
    22118076177
    Rcpt MAXCO33EMDB66576155
    Units 14.1KWH

    Token 5415 9322 5825 7106 3254

    Cost TZS 4098.37
    Serv Charge TZS 0.00
    Tax TZS 901.63
    Total TZS 5000
    eSign

    Msaada

    ReplyDelete
  32. Tanesco makao makuu tunaamba muangalie utendaji wa TANESCO KISARAWE wanatuchosha sana kwa kweli' hii ni kero kubwa sana maana kila mtu tanesco kisarawe lisemwalo lipo, mbona ofisi nyingine hazisemwi

    ReplyDelete
  33. Naomba msaada wa token. Nimenunua umeme kwa mpesa 4HP1T03WE3 Imethibitishwa. Tsh10,000.00 imetumwa kwa LUKU2-TANESCO kwenye akaunti namba 24213833031 tarehe 25/8/17 saa 7:13 PM. salio lako la M-Pesa ni Tsh138,518.00.

    ReplyDelete
  34. Mm ni mkazi wa Mabibo Dsm.Mwanzo matumizi yangu ya umeme yalikuwa makubwa kiasi maana nilikuwa ninagandisha Barafu hivyo 5000 nilikuwa ninapata unit 14.10.Baada ya kuacha biashara ya Barafu sasa hivi matumizi yangu kwa mwezi hayavuki unit 70 kiwango ambacho ni cha chini kabisa yani chini ya unit 75.Sasa swali langu nauliza nifanyeje ili niweze kurudishwa kwa watumiaji wa chini yaani @ tshs 100/unit ?

    ReplyDelete
  35. Hello Naitwa Vedasto nimenunua umeme kwa njia CRDB, sms iliyorudi token kazikutimia:
    Ref: LK171028211459632852 luku purchase TZS 5000 from AC 0152237763500. 43001488022. Meter: 43001488022
    Ref: 300211594110
    Token: 67909‎

    ReplyDelete
  36. Naitwa Vedasto. Nimenunua umeme kwa CRDB lakini token zimekuja pungufu.
    Msaada tafadhari.
    Ref: LK171028211459632852 luku purchase TZS 5000 from AC 0152237763500. 43001488022. Meter: 43001488022
    Ref: 300211594110
    Token: 67909‎

    Msaada please

    ReplyDelete
  37. Nimenunua Umeme kwa LUKU Namba 43001830066 wenye thamani ya Tshs. 200,000/- kupitia Simbanking ya NMB na Tshs. 150,000/- kupitia Simbanking ya CRDB siku ya Jumamosi Asubuhi tarehe 28/10/2017. Akaunti zote za NMB No. 22110004693 na CRDB No. 0112012421000 zimekatwa fedha lakini sijapata token zangu mpaka sasa!!!

    Tafadhali, tatizo lishughulikiwe na nipewe haki yangu haraka.


    Dr. Romanus
    0787084266

    ReplyDelete
  38. Laurent

    Napenda niwashukuru call center ya Tanesco, nimenunua umeme asubuhi,nikawa sikupata token, lakini nimewapigia simu, wamenipa token zangu fasta.
    Mko vizuri asante

    ReplyDelete
  39. Hii namba yenu 219 4400 mbona haipatikani? Limepiga zaidi ya mara 20 inampa jibu la "network busy".

    Please help urgently!

    ReplyDelete
  40. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  41. Maeneo ya Ubungo-Msewe kuna line imekata umeme toka Jana saa 1 join mpaka sasa hakuna umeme. Msaada wenu tafadhari

    ReplyDelete
  42. Jamani tanesco munakera hamupokei simu muko busy na story Ofisini. Kuna siku nilienda tanesco chumba cha dharura simu zinaita tuu hawapokei mmoja amekaa anakula chipsi mwingine anachati. Poooh! Waziri Wa nishati ona hili

    ReplyDelete
  43. Jamani tanesco munakera hamupokei simu muko busy na story Ofisini. Kuna siku nilienda tanesco chumba cha dharura simu zinaita tuu hawapokei mmoja amekaa anakula chipsi mwingine anachati. Poooh! Waziri Wa nishati ona hili

    ReplyDelete
  44. Nataka kujua hizi account za malipo zinazotolewa tanesco zinadumu kwa muda nakusudia malipo ya kuomba umeme

    ReplyDelete
  45. Umeme kufungiwa sh ngap Kwa mkoa wa mosh ikiwa unatakiwa nguzo 1 Na unapata umeme baada ya mda Gani ukisha lipia

    ReplyDelete
  46. Mina mita inauyoanzia 43.... namba zote hazifanyi kazi kasoro 3,6,9 na 0 nimekuwa nikiwapigia simu Tanesco Tegeta tangu jana mpka sasa sijapata msaada wowote

    Lawrence

    ReplyDelete
  47. Habari nimenunua umeme lakini pesa zinarudishwa ,majibu ni kwamba niwasiliane na huduma kwa wateja,kwa ajili ya kureset pini yangu ya mita,sasa nimewapigia lakini simu zinakata,naomba msaada namba yangu ya mita ni 43001327386,,namba yangu ya simu ni 0652753885

    ReplyDelete
  48. Mbona remote yangu inasumbua kuingiza umeme

    ReplyDelete
  49. Nina remote batani zake hazibonyezeki nimepata ingine lakini mafundi wakijaribu kuunganisha mawasiliano in a go ma nifanyeje

    ReplyDelete
  50. Naingiza umeme kwenye mita lakiniii umeme auingiii na nikiuliza salio I anaandika error 06

    ReplyDelete
    Replies
    1. GE.Benson Majabe hapa,kwa kwaida hiyo unakuwa umekosea token namba na Mara nyingi watu huingiza namba ya lisiti

      Delete
  51. Habari wahudumu wa TANESCO. Nimenunua umeme tangu jana mchana kila nikiingiza namba inaconnect tu umeme hauingii. Nimeripoti TANESCO Tegeta tangu jana mchana. Muda wote ukipiga unaambiwa watakuja mpaka kukakucha. Leo tangi asuhuhi nimeripoti tena Tegeta kwamba sijapatiwa huduma hadi usiku huu saa mbili sijapatiwa huduma kila nikipiga naambiwa tu watakuja. Hivi ni kweli mnatoa huduma mbaya hivyo Mita yangu ni namba 37135294801

    ReplyDelete
  52. Jamani mpaka muda huu mimi mteja mwenye mita namba 37135294801 napiga simu naambiwa tu mafundi watakuja. Kutoka Tegeta hapo mpaka Mbweni unaambiwa mafundi wanakuja kama vile wanaenda mkoani. Mnanidanganya kams mtoto. Mnitia hasara ya vitu kwenye friji na vifaranga vyangu vimekufa sababu ya giza. Kwa kweli TANESCO mheshimiwa Waziri na raisi inabidi waliangalia hili shirika. Linamwangusha. TANESCO tegeta kila mteja anayeripoti kwenu analalamikia huduma yenu. Mimi nilikuwa nasikia tu ila kuanzia jana mpaka leo nimeupata ukweli. Badilikeni muende na kasi ya raisi Magufuli. Mnamwangusha kwa kutowajali wateja wenu.

    ReplyDelete
  53. Tanesco Gongo la mboto huduma kwa wateja bado sana simu muda wote zinatumika kitu ambacho haiwezekani kuongea na mteja mmoja kwa saa nzima au siku nzima napiga namba haipatikani, nimetoa ripoti tarehe 13/10/2020 kuanzia saa 9:30 alasiri simu haipatikani muda wote inasema inatumika muda ukiipata mara moja inaita haipokelewi mpaka inakata ukipiga tena inajibu inatumika leo tarehe 16/10/2020 mpaka sasa hivi saa 10:00 alasiri natuma taarifa hii sijapata huduma mita yangu ina matatizo ya kutoruhusu umeme ripoti namba 2002 napigwa kalenda mafundi watakuja siwaoni na naendelea kupiga simu kutaka kujua tatizo nini simu namba zote mbili hazipatikani kwa kweli huduma zenu ni duni kwa wateja.

    ReplyDelete
  54. Habari
    Kwa wakazi baadhi katika ukonga Mombasa njia ya kwenda Bomba mbili,maarufu mbozi pub,tangu alhamis usiku umeme umekata Wala haujarudi mpka leo hii,hakuna taarifa kwa wateja kuhusu hitilafu ama katizo la umeme,ni jambo la kushangaza umeme unakata nyumba kadhaa ili hali majirani wakinufaika majumbani mwao,umeme huu inasemekana unatoka line ya kisarawe,we arale not sure,Ila ni umeme very stressful.Nakumbuka Mh Rais wa nchi Alisema tatizo la kukatika umeme liwe historia katika jiji hili,lakini naona haiko hivyo,hii ni kuwarudisha nyuma watu katika shughuli zao.Huwezi mkatika mtu mtu huduma bila kumpa taarifa,lakini pia siku tatu usiku na mchana hakuna umeme Tena baadhi ya nyumba ni aibu kwa shirika Hilo.Ombi langu tatizo litatuliwe haraka iwezekenavyo msomapo ujumbe huu,kabla hatujaenda mahala mwingne kwa utatuzi zaidi....

    ReplyDelete
  55. Habari, mimi ni mpangaji, hapa ninapoishi kila mpangaji ana mita yake. Tatizo ni kwamba, mita yangu inaonesha nina unit nyingi sana. Zaidi ya elfu 30 na mimi sijaingiza umeme wa kiwango hicho, je nini kimesababisha hivyo? Hofu yangu ni kuwa, ninaogopa kupewa kesi ya uhujumu uchumi wakati kosa sijafanya mimi. Naomba muongozo wenu nifanyeje?

    ReplyDelete
  56. Habari nipo gongo la mboto mombasa kama inaelekekea bombambili maeneo ya kibaoni ni wiki sas imesha hatuna umeme kila tukipigia tanesco wanasema wanakuja tuambieni shida nini jamani

    ReplyDelete
  57. Umeme haununuliki kwa njia za simu tukanunue wapi?

    ReplyDelete
  58. Umeme umekatika na umerudi kwenye nyumba za jirani kwangu tu ndio haujarudi Ila kwenye meter unaonekana kufika

    ReplyDelete
  59. Nimenunua umeme sijatumiwa token miter number 37216592669

    ReplyDelete
  60. mita yangu imezimika ghafla umeme nilinunua juzi nina unit zaid ya 46 sasa naomba msaada

    ReplyDelete
  61. Nimenunua umeme kwenye sim na nimekosea namba 1 na nishatumiwa sms ya token naweza pata msaada juu ya hili?

    ReplyDelete
  62. Nimenunua umeme lakn token nimepata lakn nikiweka kwenye mita inakataa kusoma mita namba hii.43021806948 msaada please sijuhi tatizo nin

    ReplyDelete
  63. Luku ilinunuliwa tarehe 31/12/2021 bahati mbaya msg ikafutwa kabla token haijaingizwa.Mita 43027034362 msaada kupata ile token tafadhali

    ReplyDelete
  64. Mita yangu inaandika 8888888 haisomi unit nikijaribu kuweka inagoma.mita 43015432768 msaada jamani nafanyaje ili kuweka umeme.phone no. 0757428182

    ReplyDelete
  65. Huku CHAMAZI DOVYA KWA MZALA Umeme umekatika kwa baadhi ya nyumba tangu saa 3 usiku. Mpaka sasa haujarudi. Tunaomba mtufanyie marekebisho uwake nyumba zote

    ReplyDelete
  66. Peter John Kikwale 0762942326 .Marchi 29 nilibadilishiwa mita ya luku toka no 01340715042 iliyokuwa imevamiwa na unit 75 kwenda 24311097505, kwa maelezo niliambiwa ndani ya wiki mbili yaani siku 14 nitapokea token hizo .je kwaweza kunisaidia Nipo Morogoro mjini

    ReplyDelete
  67. Peter John Kikwale 0762942326 .Marchi 29 nilibadilishiwa mita ya luku toka no 01340715042 iliyokuwa imebakiwa na unit 75 kwenda 24311097505, kwa maelezo niliambiwa ndani ya wiki mbili yaani siku 14 nitapokea token hizo .hadi SS sijapokea hizo unit je mwaweza kunisaidia Nipo Morogoro mjini

    ReplyDelete
  68. NIPENDE KUULIZA NILILIPA TANESCO KWENYE CONTROL NO KUINGIZIWA UMEMEVKWENYE NYUMBA YANGU HAPA NYAMADOKE WILAYANI ILEMELA TOKA MWAKA JANA MWEZI WA 12 NA NIKATUMIWA SMS KUWA WALE WATEJA AMBAO WAMELIPA IFIKAPO TRH 31-03-2022 WOTE WATAKUWA WAMEUNGANISHIWA UMEME LAKINI HADI KESHO SIJAONA KULIKONI AU SINA HAKI MIMI YA KUUNGANISHIWA UMEME PAMOJA NA KULIPIA?

    ReplyDelete
  69. Nimenunua umeme meter yangu imegoma kuingiza umeme naomba msaada

    ReplyDelete
    Replies
    1. Vipi umepata muongozo na mm hiyo hali imenikuta lakini mitter Ni mpya Kama wamekupa muongozo tafadhali na Mimi naomba unijuze nipate muongozo

      Delete
  70. Tafadhali naomba msaada najaribu kununua umeme (unit) lakini sifanikiwi muamala unarudi na mitter Ni mpya tafadhali msaada

    ReplyDelete
  71. Umeme umeisha kabisa najaribu kuweka inaniandikia P-cut, then error 77. Meter yangu inaanza na 242121…
    Nmejaribu kuclear error kwa kuanza na 0 then namba za meter Halaf 0 tena namba za meta then OK ila error 77 unaendelea!! Nifanyaje niko gizani

    ReplyDelete
  72. Pugu bombani,no power now over 14hrs, please assist.

    ReplyDelete