April 5, 2011

MSAMAHA WA RIBA KWA WADENI WA SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unawatangazia wateja wake wenye madeni ya umeme kuwa unatoa fursa maalum ya msamaha wa riba kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Aprili 1, 2011.

Katika kipindi hicho cha miezi mitatu wateja wenye madeni ambayo yanajumuisha riba, wataruhusiwa kulipa madeni yao bila riba kwa sharti la kumaliza kulipa deni lote katika kipindi cha miezi sita kitakachomalizika Septemba 30, 2011.

Ili upate msamaha huu wa riba kwenye deni lako la umeme, unashauriwa kutembelea ofisi ya  TANESCO ya mkoa wako ili uandikishe makubaliano ya kulipa deni hilo kwa miezi sita bila riba.

Msamaha wa riba utatolewa kwa mteja yeyote wa TANESCO nchini kote ili mradi awe amezingatia masharti haya..

Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano
TANESCO MAKAO MAKUU

3 comments:

  1. Japo sii forum yake lakini ki kwa taarifa tu kwa wahusika na kama wataona ina faa wachukuwe hatua.

    JANA MAJIRA YA SAA SABA ZA MCHANA HUDUMA YA UMEME ILIKATIKA KTK MAENEO YA RAU MADUKANI ENEO LA MANISPAA YA MOSHI MJINI.

    UMEME HUO HAUJARUDI HADI SASA NINAPO PELEKA RAARIFA HII AMBAPO NI SAA 1:14 MCHANA KWA TAREHE 8/4/2011.

    NILIPIGA SIMU SAA SITA YA USIKU WA TAREHE8/4 KUTOA TAARIFA NA NIKAJIBIWA KWAMBA HAPAKUWA NA MGAWO NAPIA HAKUKUWA NA TAARIFA YOYOTE YA DHARURA ILIYOPOKELEWA NA MPOKEAJI HAKUTAKA HATA KUJUA NI NANI AMELETA TAARIFA HII. SAA TISA ZA USIKU NIKAPIGA TENA SIMU NA MPOKEAJI WA AWALI ALINIHAKIKISHIA KWAMBA TATIZO LINASHUGHULIKIWA NISIWE NA WASIWASI.

    ASUBUHI YA LEO NIMEWASILI OFISI ZA TANESCO MKOA KILIMANJARO NA KUTOA TENA TAARIFA. NIKAAMBIWA KWAMBA HUO KWA LEO ASUBUHI NI MGWAWO.

    NAJIULIZA MGAWO UNAOTOLWA KIZANI NI MGAWO WA AINA GANI?NA ISITOSHE HAKUKUWA NA KUMBUKUMKBU YOYOTE ILE YA TAARIFA ILIYOTOLEWA JANA USIKU. NA MUHUSIKA ALIKUWA AMETOKA.
    NIKAARIFIWA KWAMBA UMEME HAUTORUDI HADI MGAWO UMALIZIKE NA NDIPO WAWEZE KUTATUA TATIZO NA MBAYA ZAIDI WANANIOMBA JINA SASA SIJUI KAMA JINA HILO LITANIRUDISHIA UMEME? NINAMPONGEZA SANA AFISA UHUSIANO WA TANESCO KILIMANJARI AMBAYE NINAMJUA KWA JINA MOJA TU LA GRACE. HUYU ANASTAHILI KUWA MENEJA HUDUMA MAANA KILA KUNAPOKUWA NA TATIZO NA AKIARIFIWA HUWA LINATATULIWA MARA MOJA BILA KUPOTEZA MUDA. KWA BAHATI MBAYA HAYUPO NA NDIO MAANA WAKAZI WA RAU TUNATESEKA. LAITI ANGALIKUWEPO KILA KITU KINGEKUWA SAWA. TUNAKUPONGEZA SANA GRACE KEEP IT UP

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. Habari TANESCO:
    Nimeupenda mfumo wa huduma za ulipaji wa gharama za umeme(LUKU)kupitia njia mbalimbali za kielectroniki.Kutokana na shida wanazozipata wateja wengi wa TANESCO kutafuta huduma za LUKU katika mtaa wetu, nimefikia rasmi uamuzi wa kutaka kuwa miongoni mwa mawakala wa kutoa huduma ya LUKU tu,na si mchanganyiko wa LUKU na huduma zingine.
    Lakini kwa bahati mbaya kila napojaribu kuulizia mawakala mbalimbali walio mitaa jirani,huniambia kuwa TANESCO,hawana dirisha la uwakala wa LUKU pekee kama uwakala wa M-Pesa tu au Ezy-pesa tu, bali kuupata uwakala wa LUKU lazima upitie makampuni jirani kama vile MAXMALIPO ambayo hutoa huduma mchanganyiko ikiwemo LUKU.
    Lengo langu ni kupata uwakala wa LUKU tu,Je,hili linawezekana kwa TANESCO ?
    na kama linawezekana kipi nahitajika kuwa nacho au nije nacho,hatua zipi natakiwa kuzifuata na kiasi gani cha mtaji natakiwa kuwa nacho mpaka kufikia natoa huduma ?
    Na kama hakuna uwakala wa LUKU pekee,nipitie wapi kwenye gharama nafuu ya mtaji,ili niupate uwapate uwakala wenye LUKU ndani yake?

    Cont : sirngoroge@yahoo.com

    ReplyDelete