August 30, 2011

MATATIZO YA MFUMO WA KUUZA UMEME KWENYE VITUO VYA LUKU


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwafahamisha wateja wake wote wanaotumia mita za LUKU kuwa tangu jana mchana (29/08/2011) kumejitokeza matatizo ya kiufundi kwenye vituo vya uuzaji umeme.  Matatizo haya yamesababisha mfumo mzima wa kuuzia LUKU kutofanya kazi.

Mafundi wa TANESCO walikuwa wanashughulikia tatizo hilo ili uuzaji umeme wa LUKU urejeshwe katika hali yake ya kawaida haraka iwezekanavyo..

Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

 


IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO


TANESCO MAKAO MAKUU

6 comments:

  1. Hizi ndizo changamoto za teknolojia na tunalazimika kuzikubali.Lakini kuna uvumi kuwa hakuna mita za luku kwa wateja wapya.
    Na wateja wapya wa Kitunda Mzinga-Tsunami wanazidi kuzishangaa nguzo za TANESCO ambazo zinazidi kuchakaa bila nyaya huku baadhi yao wakiwa wameshalipia gharama za kuunganishiwa umeme na kitengo cha huduma kwa wateja mkoa wa Ilala kinazidi kupatwa na kigugumizi cha ni lini wateja hawa watakumbukwa.

    ReplyDelete
  2. Meneja wa TANESCO wilaya Gongo la Mboto na Ofisa habari-Huduma kwa wateja mkoa wa Ilala wana kauli gani chanya kwa wateja wapya wa mradi wa mtaa wa Tsunami katika kata ya Kitunda?Ukimya wao kuhusiana na suala hili ni changamoto kwa menejimenti ya TANESCO.

    ReplyDelete
  3. Mradi wa Kitunda Mzinga-Tsunami[kwa Mzee Njovu] umekamilishwa kwa awamu ya kwanza kwa kuwekewa nguzo lakini hakuna taarifa zozote kuhusiana kazi muhimu ya kutandaza nyaya za umeme.

    Kukosekana kwa taarifa hii muhimu kwa wateja kumefanya zoezi la wateja kulipia gharama za kuunganishiwa umeme liendelee kwa mwendo wa jongoo na wale waliomaliza kulipia kuendelea kusikitishwa na ukimya wa TANESCO mkoa wa Ilala.

    Wateja wanaomba tamko rasmi kutoka TANESCO mkoa wa Ilala kuhusiana na maendeleo ya mradi huu muhimu kwa wateja wa eneo la Tsumani.

    ReplyDelete
  4. Tsunami kwa Mzee Njovu tunaendelea kusubiri nyaya za TANESCO na kamwe hatukati tamaa!!

    ReplyDelete
  5. Meneja Mkoa -Ilala;
    Hii ni kukujulisha kuwa utendaji wa ofisi yako umeendelea kuthaminiwa na wateja ndani ya mkoa wa Ilala na wilaya zake.
    Kwa niaba ya wateja wapya wa wilaya ya Gongo la Mboto eneo la Tsunami kwa Mzee Njovu nawasilisha mezani kwako shukrani zilizohanikizwa na pongezi.
    Wakati hayo yakiendelea zipo changamoto zinazohusiana na huduma kwa wateja kulingana na mazingira ya maeneo husika.Mahitaji ya umeme kwa umma ni makubwa lakini watoa huduma wa ofisi ya huduma kwa wateja wajitahidi kusogea karibu na wananchi kwa kuendelea kuwapa maendeleo ya miradi ya umeme iliyopo katika maeneo yao kwa lugha nyepesi na yenye kufahamika kwa wananchi wa kawaida.
    Changamoto kubwa kwa wateja wapya ni kusafiri hadi kufika ofisi ya mkoa wa Ilala kwa ajili malipo.Hali ya usafiri wa umma kutokea Kitunda na maeneo jirani hadi Posta-Kivukoni si njema sana hasa ukiwa na kiasi fulani cha fedha mfukoni.
    Kwa staha nahitimisha.

    ReplyDelete
  6. badra najua utasoma hata kama sio wewe atakae soma amfikishie ujumbe kuna nguzo 5 mtaan kwetu zimeoza nimewapigia simu tanesco mpaka nimechoka kila nikipiga hata ile riport numba wananizungusha sijui lengo ni nini numba ya anajiita manager 0788266006 akanipa mtu wa kunishuhulikia namba yake 0715263530.huyu dada jibu la mwisha alisema shughlikia swala la kunipa riport number sikumuelewa ila nilikubali.kila nikiwapigia hakuna anachoniambia manager zaid ya kuniambia atawapa vjana watanitafuta nguzo zimeoza waya zimeshuka kama za kuanikia ngua nguo zinazuiwa na waya zilizopo kwenya nyumba za watu kama si mali ya tanesco semeni tujue ili tujue cha kufanya.NIPO TABATA KISUKULU MLIMA WA BWANA NJIA YA KWENDA MAKOKA KANISANI my no 0784303440. nawasilisha

    ReplyDelete