April 24, 2012

HASARA KUBWA KWA TANESCO


  • Nguzo 22 zaanguka kwa upepo mkali
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limepatwa na tatizo la kuanguka kwa nguzo 22 za umeme eneo la Kipawa – Uwanja wa Ndege jijini  DSM kulikosababishwa na upepo mkali uliovuma kutoka eneo linalojengwa uwanja wa ndege wa Mwl. J.K.  Nyerere (Terminal III).


Tatizo hilo la dharura litasababisha maeneo yote ya Kipawa, Tandika na baadhi ya maeneo ya Temeke kukosa umeme kwa muda wakati mafundi wa TANESCO  wakifanya kazi usiku kucha kurejesha hali ya kawaida.

Njia hiyo ya msongo wa kilovolti 33 unatarajiwa kurudishwa kwenye hali ya kawaida mapema iwezekanavyo.

Shirika linawaomba wateja wake wote kuwa watulivu wakati mafundi wanahangaika na linatoa tahadhari kwa mtu yeyote kutogusa waya uliodondoka chini.

Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwa raia na wateja wake kwa ujumla.


No comments:

Post a Comment