April 12, 2012

TUTAWAONDOA WALIOVAMIA NJIA ZA UMEME-MKUU WA MKOA DSM


Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick. wa kwanza toka kushoto ni  Mkurugenzi Mtendeja Tanesco, Eng. William Mhando na Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum, Afande Kova.


Baada ya zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo waliokuwa wamevamia maeneo yanayozunguka mitambo ya umeme na jengo la Makao Makuu ya TANESCO (Umeme Park), kufanikiwa Kamati ya ulinzi na usalama kupitia mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Sadik zoezi hilo ni endelevu kwa maeneo yote yaliyovamiwa.

Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, Afande Charles Kenyela akitoa ripoti ya kuwatoa wamachinga kwa Mkuu wa mkoa..

Akitoa taarifa ya zoezi hilo lililoanza kufanya usiku wa kuamkia Jumanne, Kamanda wa Mkoa wakipolisi Kinondoni, Afande Charles Kenyela , alisema zoezi hilo limefanikiwa, na limefanayika kwa amani.
“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa nina furaha kukuambia kwamba hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa wala kufariki katika zoezi hili na inatokana na elimu na matangazo tuliyoitoa kabla ya zoezi kupitia ndugu zetu wa TANESCO kwa vyombo vya habari”
Kwa upande wake Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Afande Suleiman Kova alisema hawatakuwa tayari kuona wananchi wanavunja sheria za nchi, na kushauri vijana kufuata sheria bila shuruti.
“Sisi wote tunapenda kuona vijana wanakuwa wajisiriamali na wanafanya biashara katika mazingira mazuri, lakini kamwe hatuwezi kuacha wakafanya kazi katika mazingira yasiyo salama au wanavunja sheria”.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni mwenyekiti   wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa Bw Said Sadik, ameagiza uongozi wa TANESCO kuainisha maeneo yote yaliyovamiwa na kukabidhi kwa kamati yake ambayo itahakikisha inasafisha maeneo hayo. Amewaagiza wananchi waliovamia maeneo ya TANESCO kuondoka mara moja ili kuepusha usumbufu.
Aidha mkuu wa mkoa aliipongeza Kamati ya Ulinzi na Usalama na mkoa pamoja na TANESCO kwa kazi nzuri waliyoifanya katika zoezi hilo lililohusisha maeneo nje ya jengo la TANESCO Makao Makuu, stendi ya mkoa, maeneo ya barabara ya Mandela kutokea mataa ya Ubungo mpaka darajani na meneo yote ya jirani.

No comments:

Post a Comment