January 26, 2016

MKOA WA KINONDONI KASKAZINI

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
KATIZO LA  UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo.

SAA:               3:00  Asubuhi 10:00 Jioni

TAREHE:      Alhamisi, 28 January 2016

SABABU:      Kuzimwa kwa laini ya MS 1, kwa ajili ya kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kudhibiti hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:
Baadhi ya maeneo ya Masaki, Msasani, Oysterbay na maeneo yanayozunguka..

TAREHE:      Ijumaa, 29 January 2016

SABABU:      Kuzimwa kwa laini ya WAZO, kwa ajili ya kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kudhibiti hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:
Goba, baadhi ya maeneo ya salasala, Wazo, Mivumoni, Madale na maeneo yanayozunguka.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 0784 768584, 0716 768584 au namba za kituo cha miito ya simu 2194400/0768 985100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza


Imetolewa na:-         OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.
No comments:

Post a Comment