February 1, 2016

MKOA WA KINONDONI KASKAZINI





SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
KATIZO LA  UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo.

TAREHE:      3 February, 2016 (JUMATANO)

SAA:               3:00  Asubuhi 10:00 Jioni

SABABU:      Kuzimwa kwa laini ya MS 1, kwa ajili ya kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kudhibiti hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara,

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:
Baadhi ya maeneo ya MASAKI, MSASANI, OYSTERBAY na maeneo yanayozunguka..

TAREHE:      4 February, 2016 (ALHAMISI)

SAA:               3:00  Asubuhi 10:00 Jioni

SABABU:      Kuzimwa kwa laini ya MAK 4, kwa ajili ya kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kudhibiti hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara,

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:
Baadhi ya maeneo ya Mwananyamala, Makumbusho sokoni, Mchangani, Meridian, Vijana, Masai pub, Shule ya msingi Ukombozi, kituo kidogo cha Polisi cha Garden  pamoja na maeneo yanayozunguka.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 0784 768584, 0716 768584 au namba za kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na:-         OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment