Bodi
ya Shirika la Umeme Nchini TANESCO ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Dkt.
Alexander Kyaruzi Machi 2, 2019 imetembelea eneo la mradi wa ujenzi wa
kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini jijini Dar es Saam ili
kijionea hatua iliyofikiwa hadi sasa.
Kituo
cha Kurasini ni moja ya vituo vitano vilivyojengwa jijini Dar es Salaam chini
ya mradi wa kuboresha na kuimarisha miundombinu ya umeme yaani Tanzania Energy Development Access Project –TEDAP ambapo
vituo vingine vinne tayari vimekwishaanza kazi na hiki cha Kurasini ujenzi wake
unakamilika mwezi huu wa Machi, Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia
miradi, Mhandisi Emmanuel Manirabona amemueleza
Mwenyekiti huyo wa bodi na ujumbe wake.
Mwenyekiti
huyo wa bodi ambaye alifuatana na baadhi ya wajumbe wa bodi Dkt. Lugano Wilson,
Balozi Dkt. James Nzagi na Bw. David Alal, alisema “Tumeridhishwa na maendeleo
ya ujenzi wa mradi huu, mradi unatia moyo kama ujuavyo mradi huu umeanza muda
mrefu kama mlivyoelezwa na meneja mwandamizi wa miradi, lengo la mradi huu
lilikuwa ni kuboresha na kuimarisha miundombinu ya umeme mikoa ya Dar es
Salaam, Kilimanjarop na Arusha sehemu zingine tayari mradi umekamilika kipande
kilichobaki ni hiki tu cha Kigamboni.” Alisema Dkt. Kyaruzi.
Akifafanua
zaidi alisema, Dar es Salaam ilikuwa imebaki Kurasini, kuja Kigamboni na kwenda
Mbagala na kama unavyoona wakandarasi wako kazini wanaendelea kuvuta waya ili
Mbagala, Kigamboni na Kurasini viunganishwe na baada ya kuunganishwa kingine kitakachofanyika kutakuwa na laini
(njia) ya pili ya msongo wa kilovolti 33, kwa sasa laini ya kwenda Kigamboni ni
moja na tayari imeshajaa na tukiweka hii ya pili ambayo itakatisha bahari kwenye
Mkondo wa Kurasini (Kurasini Creek) itakuwa imeongeza uwezo mara mbili,
Alisema.
“Juhudi
hizi zitawapa watu wa Kigamboni umeme Murua zaidi na katika kipindi kifupi
kijacho Kgamboni mambo ya umeme yatakuwa mazuri sana.” Alitoa hakikisho Dkt.
Kyaruzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Shirika la Umeme Nchini TANESCO Dkt.
Alexander Kyaruzi, (katikati), akiwa na baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo kutoka kulia, Balozi Dkt.James Nzagi, Dkt.Lugano Wilson, na Bw. David Alal, akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea eneo la utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia ya umeme eneo la upande Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Machi 2, 2019.
Meneja Mwandamizi wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, anayeshughulikia Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona, akieleza juu ya utekelezaji wa mradi huo. |
Dkt. Kyaruzi akizungumza na waandishi wa habari |
Dkt. Lugano Wilson, Mjumbe Bodi ya wakurugenzi Shirika la Umeme Nchini TANESCO.
Balozi Dkt. James Nzagi, Mjumbe Bodi ya wakurugenzi Shirika la Umeme Nchini TANESCO.
Bw.David Alal, (wakwanza kushoto) Mjumbe Bodi ya wakurugenzi Shirika la Umeme Nchini TANESCO.
|
Mafundin wakiendelea na kazi ya kuvuta nyaya za umeme kutoka Kurasini kwenda upande wa pili wa mkondo wa Kurasini Machi 2, 2019.
Mafundin wakiendelea na kazi ya kuvuta nyaya za umeme kutoka Kurasini kwenda upande wa pili wa mkondo wa Kurasini Machi 2, 2019.
Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia
miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona, akitoa ufafanuazi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi huo wakati wa ziara ya baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO Machi 2, 2019.
Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia
miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona, akitoa ufafanuazi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi huo wakati wa ziara ya baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO Machi 2, 2019.
No comments:
Post a Comment