April 1, 2019
TAARIFA YA HUJUMA KATIKA MIUNDOMBINU YA UMEME NJIA KUU UBUNGO - MLANDIZI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake na Wananchi kwa ujumla juu ya Tukio la Uhujumu wa Miundombinu ya Umeme katika Njia Kubwa ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa 132 kutoka Ubungo kwenda Mlandizi "Tower" No. 72 lililotokea usiku wa kuamkia leo Aprili 01, 2019.
*TANESCO inaomba ushirikiano wenu ili kuwabaini wote waliohusika na tukio hili la uhalifu.*
Wataalamu wa Shirika wanahakikisha Tukio hili haliathiri upatikanaji wa huduma ya umeme kwa Wateja wetu.
*Toa taarifa katika Kituo cha Polisi kilichopo karibu, ofisi ya TANESCO au kupitia mwawasiliano yafuatayo*
Kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100
Tovuti: www.tanesco.co.tz,
*Mitandao ya kijamii*
Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,
Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/
*IMETOLEWA NA:*
OFISI YA UHUSIANO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment