Mkurugenzi
Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto), akimwelezea jambo Makamu wa Rais wa Shirika la Serikali ya Japan, linaloshughulikia uratibu wa misada ya maendeleo ya kimataifa, (JICA),
Suzuki Noriko, kuhusu hatua iliyofikiwa
na TANESCO katika uboreshaji wa miundombinu ya kupoza na kusambaza umeme
alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini jijini
Dar es Salaam, ambapo JICA inashirikana na serikali katika kukiboresha kituo
hicho.
|
Jengo jipya la kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini jijini Dar es Salaam, ambacho JICA imechangia ujenzi wake.
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Makamu
wa Rais wa Shirika la Serikali ya Japan linaloratibu Misada ya Maendeleo
laKimataifa (JICA), Bw. Suzuki Noriko ametembelea kituo kipya cha kupoza na kusambaza
umeme cha Ilala-Mchikichini kinachoendeshwa na Shirika la Umeme nchini Tanesco.
Ziara hiyo aliifanya Desemba 9, 2016 ambapo
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Felchesmi Mramba, alimtembeza kujionea
hatua mbalimbali zilizofikiwa katika uboreshaji miundombinu ya TANESCO ikiwemo jingo
na mitambo.
Ziara hiyo inakuja mwezi mmoja tu baada ya
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, kuzindua kituo cha udhibiti na usimamizi
wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar es salaam kilichoko
Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo kituo hicho cha Ilala, ni sehemu ya mradi
wa uboreshaji miundombinu ya umeme kwenye jiji hilo.
JICA na mashirika mengine ya kimataifa
yanafadhili mradi huo wa uboreshaji umeme jijini ambapo lengo ni kuwapatia
wakazi wa jiji umeme ulio bora na wa uhakika zaidi, ambapo utekelezaji wa mradi
huu umehusisha ujenzi wa kituo cha kupoza nguvu za umeme chenye ukubwa wa
100MVA (2X50MVA), 132/33KV cha City Centre, ujenzi wa mfumo wa njia ya
usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground Transmission Line) na kwa
kutumia minara (Overhead Line) ya msongo wa wa kilovolti 132 kutoka kituo cha
Ilala hadi kituo cha City Centre umbali wa Kilomita 3.4, vile vile ujenzi wa
mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission
Line) kutoka kituo cha Makumbusho hadi kituo cha City Centre umbali wa kilomita
6.67.
| |
|
Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Japan, wakimalizia kazi ya kufunga mitambo kwenye kituo hicho cha Ilala |
Mhandisi Mramba
akizungumza na mwakilishi wa JICA Tanzania Bi.Toshio Nagase
Mhandisi
Mramba, akiongoza ujumbe wa JAICA kutembelea kituo hicho.
Mhandisi Mramba akimshukuru bi Nagase baada ya kutembelea kituo hicho. Katikati ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende Mgaya.
Wataalamu wa mitambo ya umeme kutoka Japan, wakijadliana
No comments:
Post a Comment