Na Magreth Subi, Grace Kisyombe
Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO), likishirikiana na vyombo mbalimbali vya habari
nchini, limefanya ziara ya kutembelea mradi wa usambaziji wa umeme ‘Backbone’
unaoanzia Iringa na kuishia Shinyanga, mradi unaotarajia kuzinduliwa na Rais wa
Jamuhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ili kujionea jidtihada
za shirika hilo.
Mradi
wa backbone unaanzia mkoani Iringa na kupita katika mikoa ya Dodoma, Singida na
kuishia Shinyanga, ni mradi mkubwa unaoweka historia toka Tanzania imepata
uhuru 1961. Akielezea mradi huo Meneja Mradi, kutoka TANESCO, Mhandisi Khalid
Rueben James, alisema mradi huo utawanufaisha Watanzania kwa kupata umeme wa
uhakika.
Mhandisi
Khalid, alisema “mradi wa backbone utafanya ukarabati wa maeneo ya kupoozea
umeme, pamoja na kunufaisha vijiji vilivyoko katika maeneo mradi unapopita.” Mhandisi Khalid alieleza kuwa wananchi walioko
katika vijiji hivyo watapata umeme kwa gharama nafuu kupitia mfuko wa uunganishwaji
umeme vijijini (Rural Electrification Fund –REF)
Mhandisi
Khalid alisisitiza kuwa vyanzo vingi vya umeme vinapatikana Ukanda wa Nyanda za
Juu Kusini, ni pamoja na makaa ya mawe, joto ardhi, upepo na maji kutoka katika bwawa la mtera. Aidha,
alielezea kwanini waliamua kuanzia mikoa inayo athirika
kama Dodoma, Singida, Shinyanga ilikuondokana changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara.
Mhandisi
Khalid alisema, mradi huu wa usafirishaji umeme ukikamilika utasaidia
kuunganisha gridi ya taifa na gridi nyingine zikiwemo za mataifa jirani kama
Kenya, Uganda, Ethiopia na Zambia.
Gharama
za mradi wa backbone zimechangiwa na wahisani kutoka nchi mbalimbali ambao ni pamoja
na Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB), Shirika la Maendeleo
Japan (JICA), Benki ya Uwekezaji ya Nchi za Ulaya (EIB), Shirika la Kiuchumi la
Maendeleo Korea Kusini(EDCF), bila kusahau Serikali ya Jamuhuri ya Muungano
Tanzania, Kwa ujumla gharama za
kukamilisha ujenzi wa mradi huu ni dola za Marekani milioni 473.6
Mradi
huu uliosimamiwa na Tanesco ulitekelezwa na wakandarasi ambao ni makampuni
matatu ambayo ni KEC International Limimted, JYOTI Structures Ltd zote mbili
kutoka India na GSE&C and Hyosung kutoka Korea Kusini. Ujenzi ulianza rasmi
mwishoni mwa novemba 2013 na kukamilika kwa wakati ulipangwa kwa asilimia 100, alisema
Muhandisi Khalid.
No comments:
Post a Comment