December 21, 2016

ziara ya wahariri Dodoma na SingidaMwendesha mifumo ya umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kituo cha kupoza na kusambaza umeme (Zuzu Sub-station), Bw. P.H. Rashid akitoa maelezo ya kiufundi kuhusu mabadiliko ya kimfumo yaliyoletwa na mradi wa Backbone wa ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha umeme kuanzia mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Dodoma na Singida, wakati wahariri wa vyombo vya  habari walipotembelea kituo hicho. Mfumo huo mpya ambao uliwashwa kwa awamu Julai mwaka huu mkoani Iringa - Dodoma, utawashwa Desemba 21, 2016 kwa sehemu iliyobaki ya Shinyanga-Singida.
Wahariri wa vyombo vya  habari wakipatiwa maelezo ya kiufundi na wahandisi wa TANESCO kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu mkoani Dodoma ambacho kimepanuliwa chini ya mradi mkubwa wa umeme wa Backbone

Meneja Mradi mkubwa wa umeme wa Backbone, unaoendeshwa na serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi  Khalid James, (kulia), na Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji kituo cha kupoza umeme cha Kibaoni mkoani Singida wakati wa ziara ya wahariri vyombo vya  habari mkoani kutembelea mradi huo Desemba 20, 2016
Mdhibiti wa mifumo ya umeme kituo cha kupoza umeme cha Zuzu mkoani Dodoma, Bi. Itika Alexander, akiwa kazini wakati wahariri wa vyombo vya habari walipotembelea kituo hicho Desemba 20, 2016.
Minara mikubwa na ya kisasa ya kusafirisha umeme mkubwa (High tension), iliyojengwa chini ya mradi wa Backbone ikionekana kandokando ya barabara ya Dodoma-Singida
Mkuu wa kituo cha kupoza na kusafirisha umeme cha Zuzu mkoani Dodoma, Mhandisi, Joseph Mongi, akitoa maelezo ya kiufundi kuhusu hatua mpya iliyopigwa na TANESCO katika kuimarisha miundombinu ya kusafirisha umeme wa kilovolti 400 wa Backbone kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia Dodoma na Singida.
Wahariri wakipatiwa maelezo
Kituo cha Zuzu cha kuposa na kusambaza umeme
Reactors mpya zilizojengwa kwenye kituo cha kupoza na kusafirisha umeme cha Zuzu mkoani Dodoma
Baadhi ya wahariri na afisa wa TANESCO kutoka kitengo cha Mahusiano, (kulia)
Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu ambacho kimepanuliwa chini ya mradi wa Backbone

No comments:

Post a Comment