Na
Magreth Subi-Moshi
Siku ya
Wafanyakazi Dunia ambayo kila Mwaka huadhimishwa Mei 01, Kitaifa Mwaka huu
imefanyika Mkoani Kilimanjaro katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika.na
kuhudhuriwa na ma elfu ya Wafanyakazi katika Taasisi za Serikali na mashirika
TANESCO ikiwa miongoni mwa Mashirika ya Serikali ambayo Wafanyakazi wake
walishiriki.
Mgeni
Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli,
alifurahishwa na umoja na ukarimu uliooneshwa Wafanyakazi kutoka Mkoani Kilimanjaro
na sehemu tofautitofauti Nchini na kusema haijawahi tokea.
Mhe. Rais akiambatana na viongozi wa juu wa Serikali
akiwamo Makamu wa raisi Mhe. Samia Suluhu, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mawaziri na Wabunge.
Aidha,
Mhe. Raisi, alitoa ahadi tano kwa Wafanya kazi na kusisitiza suala la makundi
mawili ya vyeti feki na vyenye utatanishi
katika Taasisi mbali mabali za umma, alisema vyeti feki katika Taasisi za umma
ni elfu 9000 na vyeti vyenye utatanishi ni vyeti 1500( cheti kimoja kina tumiwa
na watu zaidi ya wawili).
Mbali
na hayo, ahadi tano alizotoa Raisi, ni pamoja na baada ya kukamilika suala la uhakiki wa vyeti Serikali itatoa ajira
eflu 52,000 kwa Mwaka wa fedha 2017/2018 unaoanza Mwezi Julai, akiongelea Bima
ya ajira alisema Serikali imeshaanza kuifanyia kazi na kuongeza kuwa Bima hiyo haitachukua
nafasi ya fao la kujitoa, na kusisitiza katika suala la uhamisho na kuwaataka Wafanyakazi
wote kutokubali kuhamishwa au kuhama mpaka pale watakapo patiwa maslahi yao.
Aidha,
alisema Serikali ya Awamu ya Tano imejitahidi na bado inafanya jitihada kubwa kuboresha
maslahi ya Wafanyakazi ili waweze kunufaika katika nyanja mbalimbali, pia
aliwaambia kutakua na ongezeko la mshahara la Mwaka na kupanda kwa vyeo kwa
Mwaka huu wa Fedha.
Alimalizia
kwa kusema Mei Mosi ya Mwaka huu ni ya kipekee Mkoani Kilimanjaro na kwa sasa Serikali
inafungua ukurasa mpya ya mahusiano baina yake na Wafanyakazi wa Tanzania na
kuwataka kutimiza wajibu kazini na si maneno na unyanyasaji wa Wafanyakazi
endapo atagundua Wafanyakazi wananyanyaswa hatolifumbia macho.
No comments:
Post a Comment