November 21, 2017

Dk. Kalemani atembelea Kiwanda cha kuzalisha nguzo za zege (Concrete poles)


Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani leo jumanne Novemba 21, 2017 akiwa Mkoani Pwani katika Wilaya ya Bagamoyo ametembelea kiwanda cha kuzalisha nguzo za zege (Concrete poles) cha  East Africa Infrustructure Engineering Ltd. eneo la kidomole, Bagamoyo.

Katika ziara yake Mhe. Waziri amesisitiza agizo lake alilolitoa la kuhakikisha kuwa nguzo zinazotumika zinazalishwa hapa Nchini.

" Nguzo tunazotumia sasa ni za miti ambazo zinaharibu mazingira lakini pia si imara kama nguzo za zege"
Alisisitiza Mhe. Waziri huku akiainisha kuwa nguzo za zege zina uwezo wa kudumu zaidi ya miaka 70.

Aidha, Dkt Kalemani alisema hivi sasa Umeme unaoingia katika gridi ya Taifa ni Megawati 1450 lakini ni nia ya serikali kuwa na Megawati 5000 kufikia 2020.

Alisifu juhudi za TANESCO za kuanzisha kampuni tanzu ya kuzalisha nguzo za zege ya Tanzania Concrete Poles Manufacturing Ltd
(TCPM).

Aliitaja miradi kama ya Stieglers Gorge( Megawati 2000) ambayo imekuja baada ya jitihada kubwa za serikali na kuiagiza TANESCO kuhakikisha kuwa nguzo za zege zinaanza kutumika kufikia mwezi Desemba mwaka huu.

"Kazi yangu ni kuhakikisha Watanzania wanapata umeme wa uhakika"
Alisema Dkt. Kalemani.

Katika ziara yake Mhe. Waziri aliambatana na Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Wataalamu wa TANESCO na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Alhaj  Majid Mwanga na Mbunge wa Bagamoyo Mhe. Shukuru Kawambwa ambao walishukuru ujio wa Waziri kwani wametaja eneo la Bagamoyo kama eneo kubwa la viwanda ambalo litahitaji umeme wa uhakika.




No comments:

Post a Comment