November 27, 2017

TAARIFA KWA UMMA



Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unawafahamisha Wateja wake 
wote na Wananchi kwa ujumla kuwa;  TANESCO  imeanza utekelezaji wa  Agizo la 
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph 
Magufuli, kuhusu kubomolewa  kwa Jengo la Ofisi za TANESCO  Makao Makuu,
 liliopo Ubungo Jijini Dar es salam. 
 
Kuanzia Jumatatu Novemba 27, 2017. Ukuta wa mbele ya jengo umesha vunjwa ,  pia  
 baadhi ya Watumishi wa Shirika wameanza kuhamishiwa katika ofisi nyingine za  
TANESCO zilizopo jijini Dar es salaam ili kupisha shughuli za ubomoaji kufanyika kwa
 usalama  zaidi.
 
Uongozi wa Shirika   pamoja na Wakala wa Majengo (TBA) wanaendelea kufanya taratibu 
zitakazo wezesha zoezi la ubomoaji wa Jengo kufanyika bila kuathiri huduma kwa Wateja wa 
Shirika.
 
Katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais.
 
 Tunapenda kuwahakikishia Wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa 
Huduma za Umeme zitaendelea kupatikana kama kawaida ikiwemo huduma ya 
manunuzi ya LUKU. 
Uongozi wa Shirika utaendelea kutoa taarifa kwa kadri zoezi hili linavyo endelea, 
 
 
                         TANESCO ‘‘Tunayaangaza Maisha yako’’ 
 
 
Kwa mawasiliano
Mitandao ya Kijamii



Imetolewa Na:  OFISI YA UHUSIANO
                               TANESCO- MAKAO MAKUU.
                                Novemba 27, 2017

No comments:

Post a Comment