Naibu Katibu Mkuu Nishati, Bw. Kheri Mahimbali amesema miradi yote ya
kimkakati ya umeme inayotekelezwa na Serikali kupitia TANESCO
itakamilika kwa wakati.
Bw. Mahimbali ameyasema hayo leo Septemba 03, 2021 katika ziara ya
Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, kukagua vituo vya kuzalisha umeme
kwa gesi vya Kinyerezi.
Amesema ziara ilijikita zaidi kwenye mradi wa Julius Nyerere, ambapo
Sekretarieti iliweza kufahamu hatua zote za kuzalisha umeme hadi
kuusafilisha.
"Leo tumewaonesha Kinyerezi complex ambayo ina Kinyerezi I, Kinyerezi I
Extension pamoja na Kinyerezi ll" amesema Bw. Mahimbila.
Ametoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inayoongozwa na Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa
inayoifanya katika kuendeleza miradi ya umeme nchini.
Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri inahitimisha leo ziara ya siku tatu
kukagua miradi ya umeme, ziara ilianzia kwenye kituo cha kupokea na
kupoza umeme cha Zuzu Jijini Dodoma, njia ya umeme itakayojengwa hadi
Chalinze na mradi wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere.
No comments:
Post a Comment