Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema ni
wakati sasa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kuanza kujiendesha
kibiashara, kwa ufanisi ili kuchangia uchumi wa Taifa.
Mhe.
Makamba amesema hayo leo Septemba 26, 2021 wakati akizungumza na
Mameneja wa TANESCO wa ngazi ya Kanda, Mikoa, Wilaya na Makao Makuu.
Aidha
Mhe. Makamba amewatambulisha Wajumbe wa Bodi ya TANESCO wakiogozwa na
Mwenyeki, Bw. Omari Issa, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Maharage
Chande, walioteuliwa Septemba 25, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Wajumbe
wa Bodi ya TANESCO waliotambulishwa ni pamoja na Bw. Nehemia Mchechu,
Bi. Zawadia Nanyaro, Bw. Lawrence Mafuru, Mhandisi Cosmas Masawe, Balozi
Mwanaidi Maajar, Mhandisi Abdallah Hashim, Bw. Abubakar Bakhresa na
Bw. Christopher Gachuma.
Mhe. Makamba amesema Bodi iliyochaguliwa ina wajumbe kutoka nyanja mbalimbali na watasaidia Shirika kufikia malengo.
"Tunataka
baada ya miaka mitatu Shirika liingie katika orodha ya mashirika bora,
yenye thamani na yanayoheshimika Afrika" alisema Mhe. January Makamba
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Bw. Omari Issa, amesema atahakikisha
Bodi inafanya kazi na kutimiza malengo yake kwa kufuatilia kwa karibu
utekelezaji wa malengo na uwajibikaji.
Mkurugenzi
Mtendaji, Bw. Maharage Chande, ameeleza vipaumbele ambavyo ni masilahi
ya rasilimaliwatu, Wateja wa Shirika na utekelezaji wa mipango, hivyo
ameomba ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wa TANESCO.
"Nimhakikishie
Mhe. Waziri tutahakikisha tunarudisha heshima ya Shirika na ufanisi
kupitia ushirikiano wenu, hakuna Shirika lolote linalotoa huduma ya
umeme zaidi yetu sisi, yamkini tuwape wateja wetu huduma wanayostahili",
" alisema Bw. Maharage Chande
Meneja
Mwandamizi Rasilimaliwatu, Bw. Francis Sangunaa, aliwahakikishia
viongozi ushirikiano kwa niaba ya wafanyakazi wa TANESCO.
Mbona wanchi awasikilizwi shida zao kama mnavyo sema bahada ya miaka mitatu shirika lihingie kwenye mashirika bora wakati kelo wanazokutana nazo azifanyiwi kazi
ReplyDelete