December 6, 2010

TANESCO NA MAENDELEO YAANZA RASMI



Bi. Badra Masoud, Meneja Mawasiliano TANESCO

  • Ni kipindi kipya TBC1
  • Kurushwa kila Jumanne saa 1:00 jioni
  •  Kuchukua nafasi ya kipindi cha Bwana umeme
Hatimaye kile kipindi cha elimu kwa umma kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu kubwa na wana TANESCO na jamii kwa ujumla kitaanza rasmi kurushwa kila Jumanne saa 1:00 jioni.

Kipindi kimepewa jina jipya la “ TANESCO NA MAENDELEO” na kitakuwa kinarushwa na televisheni ya taifa (TBC1) kwa ajili ya kuelimisha jamii na umma ujumla juu ya shughuli, huduma na vipaumbele vya shirika la TANESCO.

Mtakumbuka huko nyuma kulikuwa na kipindi cha kuelimisha umma kiitwacho “Bwana umeme” ambacho kilisitishwa kwa ajili kukiboresha na kukifanya kiendane na wakati ili kuweza kukidhi mahitaji ya wakati huu ambao kuna changamoto nyingi ndani na nje ya shirika.


TANESCO NA MAENDELEO DAIMA!

2 comments:

  1. Asanteni sana kwa kuanzisha kipindi hiki ili kutoa elimu kwa jamii .Napenda kuuliza JE KAMA JILANI YANGU ANA UMEME,NA MIMI SINA NA TUKAKUBALIANA NIWE NANUNUA LUKU NA WEKA KWAKE ILI NITUMIE JAPO KWA MUDA NIKIWA NAFANYA MIPANGO YA KUWEKA NAMI KWANGU JE NIKOSA ?

    ReplyDelete
  2. Wakazi wa viwanja vya mradi Bunju BDecember 23, 2010 at 5:23 AM

    Bunju B viwanja vya mradi tuna shida ya umeme, tuelezeni tufanye nini zaidi ya maombi ya umeme ili tuwe na mwanga usiku.
    Hela zakulipia gharama tunazo, hela za luku tunazo, sasa kazi kwenu mtuongeze kwenye "customer base" yenu, ambayo ndio msingi wa biashara yenu.
    Kazi kwenu TANESCO.

    ReplyDelete