December 7, 2010

UJENZI HOLELA CHINI YA NJIA ZA UMEME

Imetoka kwa mdau wa blog, Innocent Usangira (usangira@gmail.com).




Heshima kwenu wakuu,

Tafadhali naomba kupitia blog zenu tuwasaidie watanzania wenzetu ambao hawajui kuwa si ruhusa kiusalama kufanya shughuli yoyote ile chini ya Tanesco Transmission lines.

Nimeambatanisha picha hii ambayo nimeipiga maeneo ya Tabata
(Kinyerezi) ambako kuna makazi mengi mapya lakini uvunjaji mkubwa wa sheria hizi umeanza kufanyika. Aidha mamlaka husika, Tanesco ikiwa mojawapo hazijawaelimisha wananchi juu ya hili.

Katika picha hii wananchi hawa wanaendelea kujenga majengo ya biashara na makazi chini ya HT Line.Miaka 5 au zaidi baadaye Tanesco au Tanrods itawabomolea majengo yao.Hii ni hatari kwa uchumi wa nchi kwa kuwa ni pesa zinatumika hapa.

Aidha Tanesco wanatakiwa kufanya utaratibu wa kuweka alama za kuwataarifu wananchi kutoendelea kujenga.Watu wengi wanapoteza rasilimali zao kutokana na Mamlaka husika hazitoi elimu ya kutosha kwa wananchi na pia zimekuwa kimya uvunjaji wa taratibu.

Asante

3 comments:

  1. wakazi wa viwanja vya mradi Bunju BDecember 23, 2010 at 5:29 AM

    Wakazi wa viwanja vya mradi Bunju B said...

    Bunju B viwanja vya mradi tuna shida ya umeme, tuelezeni tufanye nini zaidi ya maombi ya umeme ili tuwe na mwanga usiku.
    Hela zakulipia gharama tunazo, hela za luku tunazo, sasa kazi kwenu mtuongeze kwenye "customer base" yenu, ambayo ndio msingi wa biashara yenu.
    Kazi kwenu TANESCO.

    ReplyDelete
  2. ha ha ha ha ha. . .yet another bizarre. . .

    Hilo Genge lenyewe nalo sasa limewekewa umeme. . .

    Kweli Tanesco wako likizo. . .miaka 5 baadaye, mtu huyu atalipwa fidia ili kupisha ujenzi wa barabara

    ReplyDelete
  3. duh. . . .
    Hii ni aibu, nimepita eneo hili hivi karibuni.vibanda katika eneo hili vimezidi kupendeza kana kwamba ndio mashindano sasa yameanza. . .

    Sijui Meneja muhusika yuko likizo au vipi

    Kazi kwenu Tanesco

    Mdau

    ReplyDelete