June 13, 2013

TAARIFA KUHUSU KATIZO LA UMEME MKOA WA TANGA

 TAARIFA KUHUSU KATIZO LA UMEME MKOA WA TANGA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Tanga linasikitika kuwataarifu wateja wake wa wilayani za Korogwe, Handeni, Lushoto na Muheza kwamba kutakuwa na makatizo ya umeme siku ya Jumamosi Juni 15, 2013 na Jumapili Juni 16,2013 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni. Sababu ni kufanya matengenezo muhimu katika laini zinazoingia na kutoka katika Kituo kipya cha sambaza umeme cha Songa. Maeneo yatakayoathirika ni: Wilaya yote ya Korogwe isipokuwa maeneo ya Hale, Segera, Michungwani, Kabuku, Mkata, Kwachaga hadi Manga. Wilaya yote ya Handeni, Wilaya yote ya Lushoto na, Wilaya yote ya Muheza Tafadhali usiguse waya ulidondoka au uliokatika, toa taarifa Ofisi yoyote ya TANESCO iliyokaribu nawe. Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


 Imetolewa na:

                          OFISI YA UHUSIANO,
                           TANESCO MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment