June 7, 2013

KATIZO LA UMEME MKOA WA PWANI

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA


 TAARIFA YA KATIZO LA UMEME – MKOA WA PWANI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Pwani kuwa kutakuwa na katizo la umeme Siku ya Jumamosi, 08 Juni, 2013 kuanzia Saa 03:00 Asubuhi hadi 10:00 jioni.  SABABU ni Kufanya matengenezo, kubadilisha nguzo zilizooza katika Line ya Msongo  wa 33KV

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Mlandizi, Kongowe, Visiga, Kwa Mathias, Kwa Mfipa, Picha ya Ndege, Maili Moja, Miembe Saba, Kiluvya, Soga na maeneo yanayozunguka.

Tafadhali usiguse waya wowote uliokatika. Mwananchi usikate mti unaogusa au kukaribia line toa taarifa TANESCO kupitia namba No. 0232402850, 0655989935; 0688359998 au Call Centre No. 2194400 OR 0786985100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
    

Imetolewa na:          OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.


No comments:

Post a Comment