December 5, 2017
Menejimenti yafanya ziara Kinyerezi II
Menejimenti ya TANESCO imefanya ziara ya kutembelea Kituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia cha Kinyerezi II Megawati 240, inayotumia Teknolojia ya "combined cycle power".
Teknolojia ya "combined cycle power " inawezesha mitambo kuzalisha umeme kwa kutumia gesi na mvuke.
Lengo la ziara hiyo ni kujiridhisha kukamilika kwa mashine namba moja kabla ya kuiingiza katika Gridi ya Taifa.
Inatarajiwa Desemba 07, mwaka huu kiasi cha Megawati 30 zinaingia katika Gridi ya Taifa.
Asilimia 15 ya gharama ya mradi zimefadhiliwa na Serikali ya Tanzania na asilimia 85 ni fedha kutoka kwa wafadhili.
Asilimia 95 ya wafanyakazi ni Watanzania.
Gharama za mradi ni kiasi cha Usd 344,059,746.00.
Ujenzi wa kituo hiki ulianza Machi 2016 na kinatarajiwa kukamilika Septemba 2018 ambapo Megawati zote 240 zitakuwa zimeingia katika Gridi ya Taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment