Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA) wa Shirika la Umeme nchini Tanesco, Demetruce Dashina Akizungumza na Waandishi mara baada ya kuimarika kwa mfumo wa kununua Umeme kwa njia Luku |
Akizungumza
mapema leo jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano (TEHAMA), Bw. Demetruce Dashina amesema kulitokea tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya LUKU wakati wa kuhamisha mfumo huo kutoka Ofisi ya zamani kwenda sehemu nyingine.
“Jana
tulikuwa tunafanya uhamisho wa mfumo wa LUKU kwende katika Ofisi zetu mpya hivyo Wateja wetu walipata usumbufu kidogo, lakini kuanzia saa saba mfumo
huo umekaa sawa na wateja wanaweza kununua umeme kama walivyokuwa wanafanya
hapo awali bila shida yoyote mara baada ya marekebisho ya kiufundi” alisema
Dashina.
Aliongeza TANESCO ilijipanga kuwahudumia wateja wake kama kawaida wakati wa kuhamisha
mitambo hiyo lakini Wananchi wengi wakapata taharuki hivyo kufanya mfumo wa
ziada kuzidiwa kutokana na watu kununua umeme kuliko kawaida.
Kwa upande
wake Kaimu Meneja Uhusiano wa Bi. Leila Muhaji amewaomba radhi Wananchi kwa
usumbufu uliojitokeza na kuwasisitiza kuwa sasa wanaweza kununua katika mifumo
iliyozoeleka.
Bi. Muhaji
amesema kuwa TANESCO inatambua umuhimu wa umeme hivyo kuwataka watanzania kuwa na Imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya
kuwahudumia kama inavyohitajika.
No comments:
Post a Comment