TAARIFA KWA UMMA
Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) linasikitika kutoa taarifa kuwa, kumetokea tatizo la
moto kwenye Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme cha 33kV Ubungo jijini
Dar es Salaam majira ya Saa 9:30 alfajiri usiku wa kuamkia Agosti 22,
2013 na moto huo ulidhibitiwa kwa ushirikiano
wa vikosi vya zimamoto vya Jiji vya Knight Support na Security Group.
Vifaa
vilivyoharibiwa na moto huo ni pamoja na waya mkubwa za umeme “Power
Cables”, Control Cables na T5 Breaker. Mafundi wa Shirika wanaendelea
na matengenezo na wameshafanikiwa kurudisha
umeme kwa baadhi ya maeneo yaliyoathirika kutokea kwenye vituo vingine
vya jirani. Hata hivyo kazi hiyo inakadiriwa kukamilika kati ya wiki
moja na nusu na wiki mbili ili kurejesha umeme kwenye hali ya kawaida.
Maeneo
yanayoathirika moja kwa moja ni Sinza, Tandale, Shekilango, Magomeni,
Ubungo, Mlimani City, TCRA, Ubungo Plaza, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Chuo cha Ardhi, Makongo, Changanyikeni,
Mabibo External, Mburahati, Manzese, Tabata, maeneo yote ya Barabara ya
Mandela Kimara, Mbezi, Kibamba na maeneo yote ya jirani.
Uongozi wa Shirika unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.
No comments:
Post a Comment