Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka |
Na Henry
Kilasila
Mkurugenzi
Mtendaji TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka amesema zoezi linaloendelea la kukata
umeme kwa wadaiwa sugu ni endelevu na amewataka wadaiwa kulipa Bili zao hasa
katika kipindi hiki cha Siku kuu za Pasaka ili kuepuka usumbufu wa kusitishiwa
Huduma ya Umeme.
Ametoa
tahadhari hiyo, Aprili 10, 2017 Ofisini kwake Ubungo Jijini Dar es Salaam,
aidha aliwashukuru Wateja ambao wameshaanza kilipa malimbikizo ya madeni yao,
na ambao wamewekeana makubaliano ya kulipa madeni kwa awamu na TANESCO.
Aliongeza
fedha Shirika linazowadai Wateja wake zinahitajika sana kuboresha miundombinu
ya TANESCO.
Akiwa katika
Mkutano huo na wana Habari, pia aliwataka Wateja na Wananchi kuwa waangalifu
kipindi hiki cha mvua kwani hutokea uharibifu katika miundombinu ya Shirika
kama kuanguka kwa nguzo ama nyaya kukatika na kuwataka kutoa taarifa TANESCO
mara moja.
Aidha kwa Niaba
ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti ya TANESCO na Wafanyakazi amewatakia
Wananchi wote Heri ya Sikukuu ya Pasaka.
Mwanzoni mwa
Mwezi Machi 2017, TANESCO ilitoa notisi ya siku kumi na nne kwa Wadaiwa ambao
wamelimbikiza madeni ya umeme ambayo iliisha Machi 22, 2017, ikiwa ni
kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli ya kuitaka TANESCO kuwakatia umeme wadaiwa sugu.
Katika agizo
hilo Mhe. Rais aliitaka TANESCO kukusanya madeni kwenye Taasisi zote inazozidai
za Serikali na Binafsi ili kuliwezesha Shirika hili kutoa Huduma kwa ufanisi.
No comments:
Post a Comment