Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Wageni kituo cha kufua umeme cha Mtera |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wadau mbalimbali alipotembelea Mtera |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka. |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kituo cha Mtera Mhandisi John Skauki |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu akiongea katika ziara yake Kituo cha kufua umeme kwa njia ya maji cha Mtera alisema amezindua kikosi kazi cha kuokoa mfumo-ikolojia wa bonde la mto Ruaha Mkuu.
Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Samia aliupongeza uongozi wa
TANESCO na Wafanyakazi wa Kituo hicho kwa kazi kubwa wanayoifanya “Niwapongeze
Mafundi na Uongozi kwa kujituma kuhakikisha tunapata umeme na kwa kufika hapa
nimejionea hali halisi”. Alisema.
Kutokana na hali halisi ya uharibifu katika mto Ruaha
Mkuu, kikosi kazi hicho kimehusisha Wizara Tano miongoni mwa hizo ni Wizara za
Nishati na Madini, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Nishati na Madini,
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Aliongeza kamati hiyo, itakapomaliza kazi itatoa
mapendekezo Serikalini na Serikali itaangalia hatua za kuchukua na kipaumbele
ili kuhakikisha maji yanatiririka katika mto huo “Tumeianza kazi ya kufufua
ikolojia katika bonde la mto Ruaha Mkuu, siamini kwenye kushindwa, maji
yatatiririka tu”. Alimalizia Mhe. Samia.
Awali akimkalibisha Mhe. Makamu wa Rais, Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji Dkt. Tito E. Mwinuka, alimshukuru na kumpongeza Makamu wa Rais kwa
juhudi zake za kulisimamia suala hili kwa kina na kuanzia kikosi kazi maalum
cha kufanya utafiti wa namna ya kurejesha ikolojia mto Ruaha Mkuu.
Kwa upande wake Meneja wa
Kituo cha kufua umeme Mhandisi John Skauki akitoa historia ya Mtera kwa kifupi
kwa Makamu wa Rais alisema Kituo hicho kilijengwa
katika awamu ya tatu ya Mradi wa Umeme Ruaha Mkuu (The Great Ruaha Power
Project) ambapo Awamu ya Kwanza ilikuwa kati ya Mwaka 1970 hadi 1975,
Bwawa dogo 125Mm3 Kidatu, Mgodi wa Kidatu, Mitambo miwili ya
Megawati 50 kila mmoja.
Awamu ya Pili ilikuwa kati ya Mwaka 1977 na 1981 ambapo
mitambo miwili ya Megawati 50 kila mmoja iliwekwa Kidatu, Bwawa kubwa Mtera 3.7Bm3
na Awamu ya Tatu ilikuwa kati ya Mwaka 1984 na 1988 ilihusisha Mgodi wa Mtera na Mitambo miwili ya Megawati
40.
Akielezea zaidi alisema ujenzi ulianza mwaka 1984
hadi 1988 na Gharama za mradi ni Dola za Kimarekani 1,580M na kuongeza mitambo
imefungwa ndani ya mgodi wastani wa mita 100 chini ya ardhi na uwezo wa
kuzalisha umeme kiasi cha Megawati 80 kwa mashine zote mbili, aidha Mtera
inachangia asilimia 14.26 kwenye mitambo
ya maji
Akitoataarifa ya ufuaji umeme alisema hutegemea
kiasi cha maji yaliyopo bwawani, yanayotakiwa Kidatu na mahitaji ya umeme
katika Gridi ya Taifa.
Utaratibu huu huongozwa na kituo cha kuendesha Gridi
ya Taifa kilichopo Ubungo Jijini Dar es
Salaam (Ubungo Grid Control Centre).
“Maji huporomoka katika njia yake (Penstock) kina
cha mita 92, huzungusha Gurudumu (Turbine) ambalo huzungusha Jenereta kwa kasi
ya mizunguko 300 kwa dakika. Baada ya kuzungusha Gurudumu, maji hupita chini ya
ardhi (tail race tunnel) umbali wa kilomita 11 na baadaye kurudia kwenye mkondo
wake wa awali” alimalizia Mhandisi skauki.
Ziara hiyo ya Mhe. Makamu wa Rais ilijumuisha wadau
mbalimbali wakiwemo Ujumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Wakuu wa Mikoa, Wakuu
wa Wilaya, Uongozi wa TANESCO na Wafanyakazi.
No comments:
Post a Comment