Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Mhandisi Tito E. Mwinuka akitoa elimu kwa Wananchi wanaoishi katika vyanzo vya maji kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira |
Na Henry Kilasila
Kikosi kazi hicho kilizinduliwa na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Mwezi Aprili Mwaka huu
alipokuwa katika ziara Mkoani Iringa na kutembelea kituo cha kufua umeme kwa
njia ya maji cha Mtera.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dk. Tito E. Mwinuka, alisema Shirika
la umeme Tanznaia (TANESCO) kama mdau muhimu linashiriki kikamilifu katika
zoezi hili kwani Mto Ruaha Mkuu ni moja ya vyanzo vya maji yanayotumika katika ufuaji
umeme katika vituo vya kufua umeme kwa njia ya maji.
Aliongeza kuwa ufuaji
umeme kwa njia ya maji ni nafuu zaidi ukilinganisha na Gesi, mafuta ama kununua
kwani uzalishaji wa unit moja ni shilingi 36 ndio maana Serikali imekuwa na
mipango endelevu ya kuwa na vyanzo vingi
zaidi.
Moja ya vyanzo vya umeme katika Gridi ya Taifa ni Ufuaji
wa umeme kwa njia ya maji ambapo vyanzo hivyo vinachangia kwa 41% katika Gridi ya
Taifa, Vituo hivyo ni Kidatu, Kihansi, Mtera, Pangani, Nyumba ya Mungu na Hale.
Ufuaji wa umeme umekuwa ukiathirika Kutokana
na hali halisi ya uharibifu katika vyanzo vya maji vinavyopeleka maji katika Bonde
la mto Ruaha Mkuu kupungua ama kukaukaa, kikosi kazi hicho kimeanzan na vyanzo
vya mto Mbukwa na mto Mtitafu vilivyopo Mkoani Njombe.
Uharibifu huo ni pamoja
na shughuli za kilimo cha umwagiliji maarufu kama (vinyungu) unaofanyika kandokando
mwa vyanzo vya maji, mabadiliko ya tabia ya Nchi yanayopelekea upungufu wa mvua,
ufugaji wa mifugo na matumizi ya maji katika vyanzo hivyo yameongezeka kutokana na ongezeko la Watu
maeneo hayo.
Madhara makubwa yanatokea
kipindi cha kiangazi ambapo Wakulima hufanya umwagiliaji kwa kutengeneza
mifereji kuelekea katika mashamba yao, hivyo kusababisha maji kukauka mto Ruaha
Mkuu.
Kitaalamu ndani ya mita
sitini (60) kutoka vyanzo vya maji hapatakiwi kufanyika shughuli za kibinadamu,
lakini zimekuwa zikifanyika ndani ya mita hizo,
hivyo imefika wakati hatua lazima zichukuliwe ili kuokoa hifadhi ya vyanzo
vya maji na kurejesha uoto wa asili ili maji yaweze kupatikana mwaka mzima
katika Bonde la mto Ruaha Mkuu.
TANESCO kwa kushirikiana na wadau wengine
wametoa elimu kwa Wakulima ya namna ya kufanya kilimo kinachoendana na uhifadhi
wa mazingira ikiwa ni pamoja na kutokufanya shughuli zakibinadamu ndani ya mita
60.
Hatua nyingine zilizochukuliwa ni upandaji
wa miti ambayo haikaushi maji na inayosaidia uboreshaji wa uoto wa asili na ukataji
wa miti aina ya miwato iliyokuwa pembezoni mwa vyanzo vya maji ambayo inakausha
maji. Zoezi hili la upandaji miti llifanyika Mwezi Februari Mwaka huu ambapo
ilipandwa miti 2600.
mto Mbukwa ambao ni moja ya chanzo cha maji katika bonde ka mto Ruaha |
No comments:
Post a Comment