April 30, 2017

TANESCO yaibuka kidedea katika maonesho ya maonesho ya wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA)

Na Magreth Subi,Moshi
Shirika la umeme Nchini Tanzania (TANESO) limeibuka kidedea katika maonesho ya wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) ambayo yamefikia kilele chake Aprili 28, 2017 Mjini Moshi.

 Mgeni Rasmi katika maonesho hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, alitoa pongeza kwa TANESCO kwa Huduma nzuri inayotolewa katika kuhudumia jamii na kuwataka Wafanyakazi kuwa na ari siku zote pamoja na changamoto wanazokutana nazo kwani changamoto ndio chachu ya maendeleo kuelekea Nchi ya Viwanda kama kauli mbiu ya Mhe. Rais inavyo sema.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mhagama alitoa shukurani kwa washiriki na kutangaza washindi katika Nyanja mbali mbali na TANESCO kuibuka mshindi wa kwanza wa masuala ya Afya na Usalama kazini mahala pa Kazi katika Sekta ya Huduma kwa Wateja.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu kitengo cha Afya na Usalama Kazini Bw. Fred Kayega alitoa maelezo ya vifaa mbalimbali vya vinavyotumiwa na Wafanyakazi kujikinga na ajali pahala pa kazi kwa Mhe. Mhagama alipotembelea banda la TANESCO kabla maonesho hayo hayajafikia hitimisho.

Baadhi ya Wafanyakazi wa TANESCO Makao Makuu, pamoja na Wafanyakazi wa Mkoani Kilimanjaro, walifurahia ushindi huo kwani utazidi kuongeza hari kwa Wafanyakazi na kufanya vizuri Zaidi katika utendaji wa Kazi.
No comments:

Post a Comment