April 27, 2017

TANESCO yaelimisha Jamii Siku ya Maadhimisho Ya Osha Mkoani Moshi






Na Magreth Subi, Moshi
Maadhimisho ya Siku ya Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) Duniani ambayo hufanyika Aprili 28 ya kila Mwaka yanaendelea Mjini Moshi.
Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu “Ongeza wigo wa ukusanyaji na utumiaji wa takwimu za usalama na Afya”  yameanza Aprili 24, 2017 yakijumuisha Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi, ambayo baadhi ni TANESCO, Acacia, Geita Gold Mine,  SSRA, Breweries na Mashirika mengine mengi.
TANESCO imeshiriki vyema chini ya Mameneja wakishirikiana na Maafisa wao kutoka Makao Makuu Mkoa wa Kilimanjaro.
Kaimu Meneja Masoko kutoka Makao Makuu, Bw. Musa Chowo alielezea kifaa cha umeme tayari kwa Wateja waliotembelea banda la TANESCO na kufurahishwa na Huduma inayotolewa pamoja na elimu waliyopatiwa.
Aidha, alielezea kifaaa cha umeme tayari  kinavyopunguza gharama hususani kwa wateja wa maeneo ya Vijijini.
 “Gharama za kifaa cha umeme tayari ni shilingi elfu 36,000/= ukijumlisha na vat elfu 27,000/= jumla yake ni shilingi 63,000/= na gharama ndogo ndogo za waya na fundi aliyesajiliwa basi umeme una waka kwako”. Alisema Bw. Chowo
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Afya Mahali pa Kazi Bw.. Fred Kayega alieleza suala zima la mfumo wa umeme kwa Wateja wote walio tembelea banda la TANESCO. “Mteja anatakiwa kufanya ukaguzi wa mfumo wa umeme kwenye nyumba yake, kila baada ya miaka mitano ilikujua kama mfumo mzima bado unafanya kazi wa ufanisi Zaidi”. Aliongeza.
Mbali na hayo, Bw. Kayega aliongelea suala zima la adhari za mashine umba(Tranfoma) na mafuta kutokana na maswali ya Wateja wengi waliotembelea banda la TANESCO, alitoa ufafanuzi kwa kusema mafuta ya tranfoma yana sifa kuu mbili moja  ukaaji wake ni muda mrefu na pili kazi ya mafuta hayo ni kupooza umeme unaoingia kutoka laini kubwa na kusambazwa kwa Wateja kutoka 33kv mpaka 11kv, lakini pia yanaadhari kwa Afya ya Binaadamu, Kwa upande mwingine alieleza pia aina ya tranfoma ambazo zinatumia joto na zinazotumia upepo kupooza umeme,na kusema kwasasa shirika limeanza kuingiza transfoma za joto za kupoozea umeme.
Aidha Mtaalamu wa Afya na Usalama Kazini, Ndugu Nelson Mnyanyi kutoka makao makuu, aliongelea kuhusu vifaa mbalimbali wanavyotumia ili kuhakikisha Usalama na Afya kwa wafanyakazi ndani ya Shirika ambavyo hutumika katika shughuli zao pindi wakiwapo katika maeneo yao ya kazia, aliongelea juu ya kifaa cha “Hand held x- ray spectrometer” kifaa ambacho hutumika kupima kiasi cha dawa iliyoingia katika nguzo kama kinakidhi au kutokukidhi kulingana na viwango “Spesifications” zilizowekwa na TANESCO, “Environmental Meter” Kifaa ambacho hutumika kupima kiwango cha kelele, joto, kiasi cha cha mwanga na kiasi cha maji yaliyopo angani “humidity’’. Kifaa kingine alichofafanua ni cha “alcohol tester” ambacho hutumika kupimia wafanyakazi kujua kama wamelewa au hapana na kwa kiwango gani mfanyakazi amelewa au hapana.
Kwaupande mwingine ,Mhandisi kutoka Idara ya Masoko Ally Koyya alifafanua juu ya matumizi bora ya nishati ya umeme majumbani kwakutumia vifaa ambavyo vinakidhi na kuleta usalama majumbani, mafunzo hayo ikiwemo aina mbali mbali za taa, jokofu, jiko la umeme,  pamoja na kufafanua uhai wa maisha ya kila kifaa na faida zake.
Hatahivyo wakazi wa Moshi mjini, walifurahishwa na Maelezo pamoja na  elimu inayotolewa, na kusema wamejifunza mengi waliyokuwa hawayafahamu kuhusu TANESCO nakuomba elimu iwekewe mkazo na jamii itapata uwelewa mkubwa kupitia wao.
Huku wakishinikiza maneno ya Mhe. Rais walioyasikia kuhusu neno “Ka-ta” na kusema kwa hali hii wanaunga mkono hoja na kwa maendeleo ya Taifa kuelekea uchumi wa viwanda.




1 comment:

  1. Good one!!.... Safety first, we light up your life.

    ReplyDelete