December 27, 2014

TAARIFA KWA WATEJA WA ARUSHA

Nguzo ya HT laini ya 11KV M2 eneo la Sekei Arusha imeanguka. Mafundi wamefungua jumper.

Maeneo yanayoathirika ni Oligli, Bangata Star TV, Visima vya maji na Midawe.

Mafundi wameanza kazi ya kubadilisha nguzo

December 9, 2014

TAARIFA KWA WATEJA WA MAENEO YA UPANGA NA AZIKIWE

 Shirika la Umeme Tanesco linawatarifu wateja wake wa maeneo ya Upanga na mtaa wa Azikiwe kuwa kumetokea shoti kubwa muda wa saa 11.30jioni baada ya Mkandarasi wa mradi wa Hifab kukata waya mkubwa wa msongo wa kilovolti 11 na hivyo kusababisha Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme cha Mjini Kati (City Centre) kuzima ghafla. Mafundi wa Karakana ya Umeme kutoka Makao Makuu wanashugulikia tatizo na tunatarajia umeme utarudi kesho mchana baada ya kuunga waya huo na kubadili vifaa vilivyoungua kwenye Kituo cha City Centre. Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza. Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano Tanesco Makao Makuu.

December 8, 2014

KATIZO LA UMEME – MKOA WA ILALA



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Wilaya ya Tabata  kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-

TAREHE:       Alhamisi 11, Disemba, 2014 na Jumatano 17 Disemba 2014  
 
MUDA:           Saa 03:00 Asubuhi hadi 11:00 jioni   
                                                 
SABABU:      Kubadilisha nguzo zilizooza na kukata miti iliyopita kwenye laini

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:

11th December 2014
Segerea, Kinyerezi, Bonyokwa, Kifuru, Bangulo na maeneo ya jirani.

17th December, 2014
Tabata kimanga, Kisukuru, Makoka,na maeneo ya jirani.

Tafadhali usiguse waya wowote uliokatika toa taarifa TANESCO kupitia namba Kitengo cha dharura ilala: 022 213 3330, 0784 768586 au namba za huduma kwa wateja 2194400 au 0768 985 100 na Kitengo cha dharura Tabata 0684 001068, 0715768589

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na:            OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.


December 7, 2014

TANGAZO KWA WATEJA WA MKOA WA ILALA

Shirika la Umeme Tanesco linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Ilala kuwa jana, saa 4 usiku kumetokea hitilafu ya dharura kwenye kituo chake cha kupooza umeme cha Ilala hivyo kusababisha ukosefu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya Kurasini, kigamboni, Mbagala, Changombe, Nyerere rd, Mafundi wa karakana ya umeme wanashugulikia tatizo na tunatarajia umeme utarudi saa 10:00 jioni leo.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

IMETOLEWA:
                        OFISI YA UHUSIANO
                          TANESCO MAKAO MAKUU

December 4, 2014

TAARIFA KWA UMMA




TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKOSEKANA KWA UMEME
KWA BAADHI YA MAENEO NCHINI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linanapenda kutoa ufafanuzi kwa wateja wake kuhusu sababu za kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya maeneo nchini kwa nyakati tofauti kama ifuatavyo:-

Mosi, Kuanzia Novemba 26, 2014 hadi Desemba 1, 2014 Mikoa yote iliyoungwa kwenye gridi ya taifa ilikuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo kutokana na kuharibika kwa mashine moja ya Mtambo wa Kufua Umeme wa Kidatu yenye uwezo wa kufua megawati 50. Mtambo huo kwa sasa umetengamaa na hakuna Mkoa wenye upungufu wa umeme.

Pili, Novemba 29, 2014 Kulitokea hitilafu ya kulipuka na kuungua kwa Kikata Umeme (Circuit Breaker) kwenye Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme cha Ubungo upande wa msongo wa kilovolti 33 na hivyo kusababisha gridi nzima ya taifa kutoka saa 11.38jioni na kurejesha saa 3.03 usiku kwa mikoa yote baada ya kutengeneza kifaa kilichoharibika. Hata hivyo baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) yaliendelea kukosa umeme kwa siku 2 mfululizo hadi tulipo funga Kikata Umeme kingine. Tatizo hilo limesha patiwa ufumbuzi na Mkoa huo kwa sasa unapata umeme kama kawaida.

Tatu, Kuanguka kwa nguzo kwa baadhi ya maeneo katika jiji la Dar es Salaam kutokana na kuanza kwa kipindi cha mvua.

Nne, Matengenezo yanayoendelea ya ukarabati wa miundombinu kwa mikoa yote ya nchini. Kazi zinazofanyika kwenye zoezi hilo kwa sasa ni kubadilisha nguzo zilizooza, kunyanyua nguzo zilizoinama, kuvuta nyaya zilizolegea na kukata miti inayogusa nyaya za umeme. Zoezi kama hili hufanyika kwa kila mkoa kwa nchi nzima kama tahadhari kabla ya kuanza kwa kipindi cha masika ambacho kinaambatana na mvua na upepo mkali.

Kwa sababu hii kubwa, kumekuwa na usumbufu wa kukatwa kwa umeme kwa baadhi ya maeneo kwa nyakati tofauti kulingana na ratiba ya mkoa husika ili kupisha zoezi hilo ambalo tunatarajia litakamilika mwezi huu wa Desemba.

Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Imetolewa na
Ofisi ya Uhusiano,

December 3, 2014

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linanapenda kutoa ufafanuzi kwa wateja wake kuhusu kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam kwa sababu mbalimbali kama ifuatavyo:-

Mosi, Kuanzia Novemba 26, 2014 hadi Desemba 1, 2014 Mikoa yote iliyoungwa kwenye gridi ya taifa ikiwemo Dar es Salaam ilikuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo kutokana na kuharibika kwa mashine moja ya Mtambo wa Kufua Umeme wa Kidatu yenye uwezo wa kufua megawati 50. Mtambo huo kwa sasa umetengamaa na hakuna Mkoa wenye upungufu wa umeme.

Pili, Novemba 29, 2014 Kulitokea hitilafu ya kuungua kwa Kikata Umeme (Circuit Breaker) kwenye Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme cha Ubungo upande wa msongo wa kilovolti 33 na hivyo kusababisha baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) kukosa umeme kwa siku 2 mfululizo. Tatizo hilo limeshapatiwa ufumbuzi na Mkoa huo kwa sasa unapata umeme kama kawaida.

Tatu, Kuanguka kwa nguzo kwa baadhi ya maeneo katika jiji la Dar es Salaam kutokana na kuanza kwa kipindi cha mvua.

Nne, Matengenezo yanayoendelea ya ukarabati wa miundombinu kwa mikoa yote ya Dar es Salaam. TANESCO inaendesha zoezi la ukarabati wa miundombinu yake kwa mikoa ya Kinondoni Kusini (Magomeni), Kinondoni Kaskazini (Mikocheni), Ilala na Temeke. Kazi zinazofanyika kwenye zoezi hilo kwa sasa ni kubadilisha nguzo zilizooza, kunyanyua nguzo zilizoinama, kuvuta nyaya zilizolegea na kukata miti inayogusa nyaya za umeme. Zoezi kama hili hufanyika kwa kila mkoa kwa nchi nzima kama tahadhari kabla ya kuanza kwa kipindi cha masika ambacho kinaambatana na mvua na upepo mkali.

Kwa sababu hii kubwa, kumekuwa na usumbufu wa kukatwa kwa umeme kwa baadhi ya maeneo mara moja kwa siku ili kupisha zoezi hilo ambalo tunatarajia litakamilika mwezi huu wa Desemba.

Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na
Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO MAKAO MAKUU.