May 29, 2015

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME MKOA WA ILALA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Ilala kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMAPILI tarehe 31/05/2015 kuanzia saa 3:00 Asubuhi hadi 12:00 Jioni.  Sababu ni kufanya matengenezo kwenye njia ya umeme ya msongo wa Kilovolti 11 na Transfoma.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:

Polisi Kati, baadhi ya maeneo ya katikati ya Jiji, Gerezani, Lugoda, Dawasco na maeneo yote ya Kamata. Maeneo ya Kariakoo, Kidongo Chekundu, Hospitali ya Mnazi Mmoja na maeno mengine ya jirani.

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: Dawati la dharura Mkoa wa Ilala - 022 213 3330, 0784 768586, 0715 76 85 86 au Kituo cha Miito ya Simu Namba 2194400 au 0768 985 100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza


Imetolewa na:   OFISI YA UHUSIANO,
                             TANESCO – MAKAO MAKUU. 
                                     

No comments:

Post a Comment