May 29, 2015

TAARIFA

KUKOSEKANA KWA UMEME BAADHI YA MAENEO YA MKOA WA KINONDONI KASKAZINI (MAGOMENI).

Shirika la umeme Tanzania linawatangazia wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini (Magomeni)kuwa imetokea hitilafu ya kiufundi kwenye kituo cha kupooza na Kusambaza Umeme cha Ubungo upande wa msongo wa kilovolti 33 leo Mei 29,2015 majira ya saa sita mchana na hivyo kusababisha baadhi ya maeneo kukosa umeme.

Maeneo yanayokosa umeme ni: Makoka,Mbezi Luis, Kibamba, Makabe, Mpiji, Gpba Juu, Malamba Mawili, Kibwegere,Ubungo, Mabibo,Baadhi ya Maeneo ya Sinza Makaburini na Kibangu.

Mafundi wanabadilisha kifaa kilichoungua na umeme unatarajiwa kurudi leo saa 3 usiku.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.

No comments:

Post a Comment