May 21, 2015

TAARIFA

KUKOSEKANA KWA UMEME KWA MIKOA YA DODOMA, SINGIDA, TABORA,SHINYANGA,MWANZA,NA MUSOMA.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)linaomba radhi wateja wake wote wa DODOMA,SINGIDA,TABORA,MWANZA,NA MUSOMA kwa kukosa umeme kuanzia jana usiku saa 3:06 Mei 20,2015 kutokana na hitilafu ya kiufundi kwenye njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 220 kutoka Mtera kwenda Dodoma.

Mafundi wa Tanesco wapo eneo la tukio kuanzia jana usiku hadi sasa wanaendelea na kazi ili kuondoa hitilafu hiyo.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
Tanesco Makao Makuu.

No comments:

Post a Comment