July 24, 2015

TAARIFASHIRIKA LA UMEME TANZANIA

       TAARIFA YA KUKATIKA KWA UMEME JIJI LA DAR ES SALAAM

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwajulisha wateja wake wa mkoa wa Dar es salaam kwamba kuna hitilafu imetokea katika baadhi ya mitambo 


katika kituo cha kupoozea na kusambaza umeme cha Ubungo na kupelekea jiji lote la Dar es salaam kukosa umeme majira ya saa tano asubuhi leo tarehe 24/07/2015.

Jitihada za kurekebisha tatizo hilo zinaendelea na tayari umeme umeshaanza kurejea katika hali yake ya kawaida na hadi kufikia saa kumi jioni umeme utakuwa umerudi katika maeneo yote ya jiji la Dar es salaam.

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.Imetolewa na:   OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment