July 25, 2015

TAARIFA

TAARIFA YA KUKOSEKANA UMEME  KWA MUDA KWA BAADHI YA MAENEO YA JIJI LA DAR ES SALAAM NA ZANZIBAR.

Shirika la umeme la Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wa baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na Zanzibar kuwa kutakuwa na zoezi la kubadilisha moja ya kifaa kilichoungua jana kwenye kituo cha kupoozea na kusambaza cha Ubungo leo Julai 25,2015 kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 10:30 jioni.

Hivyo wakati zoezi hilo linaendelea baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na Zanzibar yatakosa umeme.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.

No comments:

Post a Comment