July 24, 2015

TAARIFA


TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO YA JIJI LA DAR ES SALAAM

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linaomba radhi kwa wateja wake wa baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam kwa kukosa umeme leo, Julai 24, 2015 majira ya saa 5 asubuhi kutokana na hitilafu ya umeme kwenye kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Ubungo na hivyo kusababisha baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam kukosa umeme.  Mafundi wameendelea na kazi hiyo na umeme umerejea katika hali yake ya kawaida majira ya saa 10:30 jioni.


Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Imetolewa na:   Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO Makao Makuu.
2 comments:

  1. Arusha ni wiki sasa mnakata tu hamna namna nyingine

    ReplyDelete
  2. Arusha ni wiki sasa mnakata tu hamna namna nyingine

    ReplyDelete