July 23, 2015

TAARIFA YA UBORESHAJI WA MFUMO WA LUKUShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linafuraha kuwajulisha wateja wake kote nchini wanaotumia mfumo wa LUKU kwamba kuanzia Agosti 1 mwaka huu tutahamia kwenye mfumo mpya wa LUKU ulioboreshwa zaidi.

Mfumo huo ambao umeboreshwa utakuwa na kasi zaidi, utaweza kuhudumia idadi kubwa ya wateja kwa wakati mmoja na utaondoa usumbufu wowote ambao ulijitokeza kwenye mfumo wa awali.

Hivyo wakati wa kuhamia kwenye mfumo huo mpya tutasitisha huduma ya kununua umeme kwa wateja wa LUKU usiku wa kuamkia Agosti 1, 2015 kwa muda wa saa 24.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote ambao unaweza kujitokeza.


TANESCO: “Tunayaangaza Maisha Yako”


Imetolewa na:   OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment