February 18, 2016

TAARIFA MKOA WA TEMEKE

                                       SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
     
  TAARIFA  YA LORI KUGONGA NGUZO MKOA WA TEMEKE ENEO LA KIZINGA.

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)linawataarifu wateja wake wa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Temeke kuwa usiku wa kuamkia leo Februari 18,2016 kuna lori limegonga nguzo ya umeme maeneo ya Mto Kizinga kwenye line ya Mbagala.Nguzo hiyo ilipogongwa iliangukia line ya maweni.Hivyo maeneo yafuatayo yanakosa umeme:

Kijichi na Maweni.Mafundi wanashughulikia kuibadilisha nguzo hiyo ambayo pia imeungua moto.

Imetolewa na ofisi ya Uhusiano,
Tanesco Makao Mkuu.

No comments:

Post a Comment