February 5, 2016

TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MIKOA.TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MIKOA ILIYOUNGWA KWENYE GRIDI YA TAIFA FEBRUARI 7, 2016

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa mikoa ya Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Musoma, Mara, Babati, Simiyu na baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga kuwa yatakosa umeme siku ya JUMAPILI tarehe 7 FEBRUARI, 2016 kuanzia Saa 1:00 Asubuhi hadi Saa 11.00 Jioni.

Sababu ni kazi inayoendelea kufanywa na Mkandarasi anayejenga njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo mkubwa wa kilovoti 400, maarufu kama ‘Backbone’ kutoka Iringa kwenda Shinyanga.

Mradi huo unalenga kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini na utekelezaji wake upo katika hatua za mwisho.

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na:        OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU.

 

No comments:

Post a Comment