Dkt. Kalemani alisema lengo la ziara hiyo ni kukabidhiwa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumie mvuke baada ya kuwa umekamilika.
Aliongeza mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya mvuke ni wa kwanza kwa Afrika Mashariki na kusema utazalisha kiasi cha Megawati 4.2 ambazo zitaingia kwenye gridi ya Taifa.
"Baada ya mwezi tutazalisha Megawati nyingine 40.2 kutoka katika mashine itakayotumia mvuke kuzalisha umeme". Alisema Dkt. Kalemani.
Mradi wa Kinyerezi II utakapokamilika utaingiza kiasi cha Megawati 248 kwenye gridi ya Taifa.
Mitambo sita ya mradi wa Kinyerezi ikikamilika miezi miwili kabla ya muda wa mkataba wake kuisha na mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mvuke umekamilika siku 21 kabla ya mkataba wake.
Mtambo wa mwisho wa kuzalisha umeme kwa kutumia mvuke unatarajiwa kukamilika mapema mwezi wa nane na utazalisha Megawati 40.2.
Aidha, kutokana na mradi kukamilika kwa haraka Serikali imeokoa kiasi cha fedha milioni 9.8 dola za Marekani, ambapo Dkt. Kalemani alitoa agizo ya fedha hizo zitumike kwenye kuimarisha miundombinu.
Mradi wa Kinyerezi II unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na wafadhili Benki ya watu wa Japani.
Gharama za mradi huu ni Dola 344, Tangu Februari mwaka huu Serikali ya Tanzania imelipa fedha zote zilizotakiwa ambazo ni kiasi cha dola za kimarekani milioni 51.6.
Mradi umefikia asilimia 96 kukamilika kazi zilizo baki ni za ujenzi wa barabara na nyumba za Wafanyakazi ambapo Mheshimiwa Waziri ameagiza kufikia mwezi Septemba ziwe zimekamilika.
No comments:
Post a Comment